Home WANAWAKE NA MAENDELEO MYWO yafanya ziara ya kihistoria Tanzania

MYWO yafanya ziara ya kihistoria Tanzania

0 comment 130 views

Kikundi cha maendeleo ya wanawake kutoka Kenya (MYWO) kimefanya ziara ya kihistoria nchini Tanzania.

Kikiongozwa na Mwenyekiti wake, Bi. Rahabu Mwikali pamoja na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mh. Dan Kazungu walimtembelea Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Dar es Salaam na kumpatia zawadi mbalimbali zikiwemo picha na mavazi asili.

Wageni wengine waliokuwepo ni Bi. Getrude Mongella ambaye ni mwanasiasa mkongwe Tanzania na alikua Rais wa kwanza wa Pan African Parliament (2004-2009) na Bi. Muthoni Likimani ambaye ni mwanasiasa mkongwe kutoka Kenya.

MYWO kilianzishwa mwaka 1952 kikiwa na lengo la kuhamasisha maendeleo ya wanawake.

Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu, akisalimiana na Mama Maria Nyerere wakati wa zaira ya kihistoria yaliyofanywa na kikundi cha Kenya Maendeleo ya Wanawake Organization (MYWO) ambacho kilianzishwa mwaka 1952 kwa ajili ya kuhamasisha umoja na maendeleo ya wanawake, nyumbani kwa Mama Maria Nyerere, jijini Dar es Salaam, hivi karibuni. Aliyeketi kulia ni mwanasiasa mkongwe kutoka kenya, Muthoni Likimani, na wa kwanza kushoto ni mwanasiasa mkongwe wa Tanzania na Rais wa kwanza wa Pan-African Parliament (2004-2009),Gertrude Mongella.

Mama Maria Nyerere (Katikati) akipeana mkono na mwanasiasa mkongwe kutoka kenya, Muthoni Likimani kama ishara ya kumshukuru kwa zawadi walizoleta kutoka Kenya, wakati wa ziara ya kihistoria yaliyofanywa na kikundi cha Kenya Maendeleo ya Wanawake Organization (MYWO) ambacho kilianzishwa mwaka 1952 kwa ajili ya kuhamasisha umoja na maendeleo ya wanawake, nyumbani kwa Mama Maria Nyerere, jijini Dar es Salaam, hivi karibuni. Wa kwanza kushoto ni mwanasiasa mkongwe wa Tanzania na Rais wa kwanza wa Pan-African Parliament (2004-2009),Gertrude Mongella.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter