Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Nukuu (Quotes) 20 za mafanikio

Nukuu (Quotes) 20 za mafanikio

0 comment 341 views

Maneno yana ushawishi mkubwa katika kuhamasisha watu kuendelea kusonga mbele na kutokata tamaa. Kuna wakati unaweza kujikuta umekwama na hujui jinsi gani ya kukabiliana na changamoto zilizopo. Siku zote, kumbuka kuwa changamoto tunazopitia ni sehemu ya maisha yetu na japokuwa zitatupitisha katika wakati mgumu, tunapaswa kuzitumia kujifunza na kuwa bora zaidi ili kuepuka kurudia makosa kwa mara ya pili.

Kila mmoja wetu ana malengo ya ndoto zake lakini licha na kutofautiana, lengo letu wote ni kuendelea kupigania malengo hayo na hatimaye kufanikiwa.

Hizi ni Nukuu/Quotes 20 kutoka kwa watu mbalimbali duniani kuhusu mafanikio. Bila shaka zitakuhamasisha kuendelea kufanya kazi kwa bidii bila kukata tamaa.

NUKUU:

Kisasi kizuri ni mafanikio.

– Frank Sinatra

Fursa zina aibu, zinakusubiri uzikimbilie.

– Reginald Mengi

Ota ndoto kubwa na thubutu kushindwa.

– Norman Vaughan

Hatua ya kwanza ya mafanikio ni matamanio.

– Napoleon Hill

Ili kufanikiwa ni lazima tuamini kuwa tunaweza.

– Nikos Kazantzakis

Mafanikio ni pale ambapo maandalizi na fikra vinakutana.

– Bobby Unser

Anzia ulipo. Tumia kile ulichonacho. Fanya kile unachoweza.

– Arthur Ashe

Kila siku, ninajitahidi kufanya vizuri kuliko nilivyofanya jana.

– Reginald Mengi

Ndoto zetu zinaweza kuwa kweli ikiwa tuna ujasiri wa kuzitimiza.

– Walt Disney

Mtu ambaye hajawahi kufanya kosa hajawahi kujaribu kitu kipya.

– Albert Einstein

Ukitazama kwa karibu, mafanikio ya usiku mmoja huchukua muda mrefu.

– Steve Jobs

Mafanikio huja kwa wale ambao wanafanya bidii kuyatafuta.

– Henry David Thoreau

Huwezi kuvuka bahari kama huna ujasiri wa kuacha kuona ufukwe.

– Christopher Columbus

Mafanikio ni kupita kutoka aina moja ya kushindwa hadi nyingine bila kukata tamaa.

– Winston Churchil

Kufahamu pekee haitoshi, ni lazima tuweke kwenye matendo, Kutamani haitoshi, ni lazima tufanye.

– Johann Wolfgang

Mafanikio si vitu ulivyokamilisha katika maisha yako, ni nini ulichowahamasisha wengine kufanya.

-Unknown (Aliyesema maneno haya hajulikani)

Hakuna siri ya mafanikio, ni matokeo ya maandalizi, kufanya kazi kwa bidii na kujifunza kutokana na kushindwa.

– Colin Powell

Kama unataka kufanya kitu, utatafuta njia. Kama hutafanya hivyo, utatafuta kisingizio.

– Jim Rohn

Siwezi kukupa kanuni ya mafanikio, lakini ninaweza kukupa kanuni ya kushindwa, nayo ni kujaribu kumridhisha kila mtu.

– Herbert Bayard Swope

Mafanikio sio ufunguo wa furaha. Furaha ni ufunguo wa mafanikio. Kama unapenda unachofanya, utafanikiwa.

– Albert Schweitzer

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter