Home AJIRA Fanya hivi kama unafikiria kujiajiri

Fanya hivi kama unafikiria kujiajiri

0 comment 99 views

Changamoto ya ajira imekuwa moja kati ya matatizo makubwa hapa nchini. Kundi kubwa la watu hasa vijana wamekwama kimaisha kutokana na kukosa ajira japokuwa wamefika hadi ngazi za juu katika elimu. Kama unafikiria kuwa mjasiriamali ili kupiga vita umaskini, mbinu zifuatazo zinaweza kuwa mwanga katika kufanya hilo ili upate nafasi ya kutengeneza kipato

  • Anza na unachokijua au unachokipenda
  • Tumia elimu na maarifa uliyonayo
  • Angalia mazingira na kuwa mbunifu
  • Jitangaze kidogo kidogo
  • Omba ushauri pale unapokwama
  • Zingatia utoaji bora wa huduma
  • Endesha biashara nyumbani kuokoa gharama
  • Bana matumizi na wekeza katika biashara
  • Kuwa mvumilivu na fanya kazi kwa bidii
  • Kuwa mtafiti/mfuatiliaji
  • Usichoke kujifunza na kujiendeleza
  • Usikate tamaa

Changamoto mbalimbali zimepelekea biashara ndogondogo kuwa kimbilio la watanzania walio wengi. Ni fursa ya kujiingizia kipato na kukabiliana na ugumu wa maisha.  Unaweza kutumia mbinu za hapo juu kama muongozo wa kuanzisha biashara yako na kisha kuikuza kadri siku zinavyokwenda.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter