Home AJIRA Mradi wa dola 10.6m kusaidia vijana wazinduliwa

Mradi wa dola 10.6m kusaidia vijana wazinduliwa

0 comment 124 views

Rais Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amezindua mradi wa Kijana Nahodha wenye thamani ya dola za Kimarekani Milioni 10.6 ambao umedhaminiwa na Shirika la Misaada la Watu wa Marekani (USAID).

Mradi huu una lengo la kuwawezesha na kuwapa ujuzi vijana katika sekta mbalimbali ikiwemo ujasiriamali wa kilimo, ufugaji, utalii, uchumi wa buluu, stadi za maisha na afya kwa vijana.

Vile vile mradi huu umelenga kuwafikia Vijana 15,000 wenye umri kati ya miaka 15 hadi 25 Unguja na Pemba.

Rais Mwinyi amesema mradi huu wa vijana ni miongoni mwa vielelezo vya kuwepo kwa ushirikiano wa dhati kati ya Marekani na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizindua mradi huo, Rais Mwinyi amezitaja changamoto zinazowakabili vijana kuwa ni pamoja na ukosefu wa ajira, matumizi ya dawa za kulevya, mimba na ndoa za umri mdogo.

Nyingine ni ugonjwa wa Ukimwi, afya ya akili, ukatili na udhalilishaji wa kijinsia yakiwemo matumizi mabaya ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter