Home WANAWAKE NA MAENDELEO Uwekezaji afya mama na mtoto wahitajika

Uwekezaji afya mama na mtoto wahitajika

0 comment 198 views

Uwekezaji katika kuboresha huduma ya afya ya mama na mtoto na sekta ya afya kwa ujumla ni mambo ya muhimu na ya lazima katika kutokomeza fistula nchini.

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT Brenda Msangi amesema hayo katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kutokomeza fistula ya uzazi duniani.

“Katika kipindi cha miaka 20 kama nchi kwa kiasi fulani kuna mafanikio ya kujivunia kwani wanawake zaidi ya 17,000 wamepatiwa matibabu ya fistula na kati ya hao CCBRT imechangia kwa zaidi ya 50%.

Katika hili tunaishukuru sana serikali yetu ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ambae pia ni balozi wa kutokomeza fistula, wadau wetu ndani na nje ya nchini kwa kuendelea kutushika mkono kufanikisha matibabu,” ameeleza Msangi.

Brenda amesema pamoja na hayo, CCBRT ina kitengo maalumu cha mafunzo kwa wanawake waliopata matibabu chenye lengo la kuwawezesha kiuchumi na kuweza kurejea kwenye jamii zao wakiwa wenye kujiamaini baada ya unyanyapaa na sonona ya muda mrefu.

Inakadiriwa kila mwaka hapa nchini wanawake 2500 hadi 3000 wanapata fistula. Juhudi za pamoja za kutoa matibabu kwa kina mama hwa wanawake ni wastani wa wanawake 1000 hivyo wanawake zaidi ya 2000 hubakia wakitaabika na ugonjwa huu wa aibu unaozuilika na kutibika.

“Kila mmoja wetu anaomchanga katika kutokomeza gonjwa hili.

Tunapoendelea kushikwa mkono na wahisani mmbalimbali kutoka nje ni jukumu letu kama Watanzania kwa kushirikiana na serikali kuhakikisha tunaboresha huduma ya afya ya mama na mtoto ili kuzuia tatizo hili kutokea,” amesisitiza Msangi.

Kauli mbiu ya mwaka huu inasema “Miaka 20 ya mapambano dhidi ya fistula jitihada zaidi zinahitajika, chukua hatua sasa tutokomeze fistula ifikapo 2030”.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter