Home AJIRA Njia sahihi ya kuandika barua pepe

Njia sahihi ya kuandika barua pepe

0 comment 379 views

Mawasiliano yamerahisishwa kwa asilimia kubwa kutokana na maboresho ya teknolojia. Wafanyakazi wamekuwa wakiwasiliana kwa urahisi ofisini na hata nje ya ofisi kupitia barua pepe. Lakini je, kila mfanyakazi anafuata njia sahihi za uandishi wa barua pepe rasmi za kikazi? Kuna utofauti mkubwa kati ya barua pepe za kirafiki na za kikazi. Katika barua pepe za kirafiki, mhusika anaweza kuandika bila kikomo huku barua pepe za kikazi zinatakiwa kuandikwa kwa ustadi lakini kwa kifupi ili mradi ujumbe iliokusudiwa kutumwa umeelezwa katika barua pepe hiyo.

Ni mambo gani mtu anatakiwa kuzingatia katika uandishi wa barua pepe?

Kwanza ni kichwa cha habari kinachoelezea mada husika. Mara nyingi watu huangalia vichwa vya habari na kufanya maamuzi ya kusoma au kuacha barua pepe hivyo kwa kuandika kichwa cha habari kilichojitosheleza unakuwa na uhakika wa kupata mrejesho kutoka kwa mpokeaji. Lengo la ujumbe huo linatakiwa kuandikwa katika kichwa cha habari kwa mfano RE (Yahusu): Kikao Cha Pili Kuhusu Masoko.

Kitu kingine muhimu katika barua pepe ni salamu rasmi. Imekuwa kawaida kwa watu wakiondoa salamu katika barua pepe lakini salamu inaweza kusaidia watu kujua kwa urahisi ujumbe unaelekezwa kwa nani, hasa kama ujumbe huo umetumwa kwa watu weng kwa wakati mmoja (Cc, Bcc). Pia epuka kujibu kila mmoja bali wale wanaohusika na meseji unayotaka kuituma.

Bainisha ujumbe na tumia lugha rasmi.  Hapa sasa mhusika anatakiwa kuandika lengo la ujumbe huo kwa lugha rasmi, na kwa ufupi . Hapa mwandishi anatakiwa kutumia tenzi sahihi na maneno yasiyo na maana nyingi ili kuepuka kupeleka ujumbe tata. Ukimaliza hapo funga mada.  Baada ya kukamilisha maudhui inashauriwa kukamilisha mada kulingana na ujumbe unaoutuma. Kwa mfano, unaweza kuweka wazi kuwa unategemea kupata majibu ya haraka au kama unataka kupata ruhusa eleza hivyo, kama unataka kupata maoni basi ainisha hivyo baada ya kukamilisha maudhui.

Mwisho,hakikisha ujumbe wako kabla ya kutuma. Kwa kuhakikisha ujumbe unapata wakati wa kurekebisha vitu ulivyokosea, kuweka viambatanisho na kuhakikisha ujumbe wako unatumwa kwa watu sahihi.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter