Home AJIRA Njia sahihi ya mawasiliano kazini

Njia sahihi ya mawasiliano kazini

0 comment 200 views

Mawasiliano husaidia mambo yaende sawa na katika mtiririko sahihi. Kila sehemu huwa kuna namna ya kuwasiliana. Huwezi kutumia lugha unayotumia mtaani kazini au katika maeneo rasmi, kwa kufanya hivyo unaweza kuingia matatani aidha kwa kuondolewa mahali husika mfano kazini, kuandikishwa barua (ushahidi tosha kwa makosa ya baadae), au kujishushia hadhi yako.

Hivyo hizi ni baadhi ya njia sahihi ya kuwasiliana ukiwa katika eneo la kazi:

Ni muhimu sana kufahamu itifaki kazini kwako, hii itakusaidia kujua ni mtu gani ambaye unatakiwa kuwasiliana nae kuhusu mambo yako. Si sahihi kupeleka mambo yako katika idara isiyohusika kwanza utaonekana hauko makini, pili utaonekana ni mtu unayependa kusambaza taarifa kazini jambo linaloweza kusababisha watu wahisi kuwa unaweza kutoa taarifa za ofisi nje ya ofisi. Hivyo ikiwa una jambo lako jitahidi kufahamu vizuri muhusika anayehusika na maswala hayo na jinsi alivyo ili kuweza kujiandaa vizuri na kuleta suluhu katika jambo hilo.

Huwa wanashauri kutofanya maamuzi ukiwa na hasira sana au furaha sana kwasababu watu wengi hujutia pale hisia hiyo ikiisha. Hivyo jitahidi kukumbuka hilo hata ukiwa unataka kufanya mawasiliano kazini. Hata kama umeudhika kiasi gani au hujapenda kitu na ukaambiwa ujielezee aidha kwa mdomo au maandishi jitahidi kuwa katika hali ya utulivu ili unayemuelezea aweze kukuelewa na kutoa suluhisho lakini kuongea kwa hasira, lugha zisizofaa hakutokuletea suluhisho la malalamiko au changamoto iliyokukuta.

Kuna muda inaweza kutokea kwamba unatakiwa kutoa maelezo kuhusu jambo fulani ukiwa kazini. Jitahidi kueleza ukweli  na kusimama katika upande mmoja. Ikiwa umesikia mambo kuhusu swala hilo lakini hauna uhakika basi usielezee mambo hayo kwasababu hata ukiombwa ushahidi utakuwa huna hio inaweza kukuletea shida. Hivyo eleza ukweli, eleza mapungufu na upande unaosimama kuhusu swala husika.

Jambo la muhimu zaidi ni kusimamia haki siku zote, hata kama watu wengine watachukizwa na ukweli uliosema lakini hio itakua ni jambo zuri kwako. Kwa sababu muda mwingine bosi wako atakuuliza jambo ambalo tayari anajua ukweli  kuhusu mfanyakazi mwenzio au maswala mengine ili kutaka tu kujua kama wewe ni mkweli au la.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter