Rais John Pombe Magufuli amesema serikali inatarajia kuajiri walimu wapya 5,000 ili kuimarisha sekta ya elimu.
Amesema tangu aingie madarakani, serikali yake imeshaajiri zaidi ya walimu 30,000 na hivi karibuni walitangaza nafasi za ajira 8,000 na sasa wanatangaza nafasi za walimu 5,000.
Alisema wanataka suala la elimu lizingatiwe nchini akisisitiza kuwa taifa lolote linalothamini elimu ndiyo linalothamini maendeleo ya kweli.
“Katika kipindi cha miaka mitano, kumetumika kiasi cha Sh. Trilioni 1.1 kushughulikia suala la elimu na tunaendelea kufanya hivyo. Katika elimu ya juu tumetumia zaidi ya Sh. Bilioni 450 kwa kila bajeti ya kila mwaka,” alisema rais Magufuli.
Rais pia alionya kuhusu utovu wa nidhamu miongoni mwa wanafunzi, akidokeza kuwa angetamani adhabu ya viboko iendelee mashuleni.
Alisema “najua hilo hamtalipenda lakini hiyo ndio njia pekee ya kumsaidia mtoto, lakini najua watoto wangu ni wapole na wanafuata masharti yote, hao viboko havitawahusu.