Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Ummy Mwalimu, ameongeza siku tano kwa waombaji wa kazi za elimu na afya kutuma maombi.
Sasa, mwisho wa kuomba ajira hizo ni Mei 28 ambapo awali ilikuwa ni Mei 23.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano katika Wizara hiyo, Mteghenjwa Hosseah amesema Waziri Ummy ameongeza siku hizo ili walioshindwa kukamilisha maombi yao tangu kutangazwa kwa ajira hizo Mei 09 watumie muda huo wa nyongeza kukamilisha.
Amesema “hadi Mei 21 saa 05:59 usiku waombaji wapya waliojisajili kwenye mfumo wa kada ya afya walikuwa 49,975 huku waliohakiki taarifa za awali wa kada ya elimu wakiwa ni 78,808 na jumla sasa maombi yote yaliyopokelewa kwa ukamilifu katika kada ya afya ni 31,673 na elimu ni 89,958.”