Mkurungenzi wa kampuni ya Mohammed Builders inayojenga soko na stendi jijini Dodoma, Mohammed Jafferji amesema mradi wa ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi pamoja na soko la kisasa unategemewa kuzalisha ajira zaidi ya 500 ambazo zitakazowanufanisha wakazi wa jiji hilo.
Jafferji amesema pamoja na ajira za moja kwa moja pia miradi hiyo itanufaisha watu wengine kama mamalishe watakaotoa huduma ya chakula kwa wafanyakazi wa miradi hiyo.
“Hatuwezi kuchukua watu wa kazi kutoka mbali tutatoa kipaumbele kwa wananchi walipo hapa jirani kwanza ili waweze kunufaika na uwepo wa miradi hii miwili”. Ameeleza Jafferji.
Alisema pamoja na ajira za moja kwa moja pia miradi hiyo itanufaisha watu wengine kama mamalishe ambao watatoa huduma ya chakula kwa wafanyakazi wa miradi hiyo. Kampuni hiyo tayari imeanza hatua za awali za ujenzi kwa kuchimba mashimo ya nguzo za jengo kuu, huku hatua inayofuata ikiwa ni kuanza ujenzi na hadi sasa hawajapata changamoto ya kuibiwa vifaa vya kazi kutokana na wenyeji kushiriki katika ulinzi wa vifaa hivyo.