Home AJIRA Unafanya kazi zako nyumbani? Zingatia haya

Unafanya kazi zako nyumbani? Zingatia haya

0 comment 130 views

Kufanya kazi kutoka nyumbani kuna faida mbalimbali lakini hiyo haimaanishi kuwa ni rahisi kama watu wanavyofikiria. Unapokuwa nyumbani mara nyingi unakuwa umejitenga na hivyo hali hiyo inaweza kuleta upweke na kupelekea kushindwa kutimiza majukumu yako kwa wakati. Mbali na hayo, unaweza kuwa na mambo mengi ya kufanya nyumbani hivyo unajikuta unapata muda mchache tu wa kufanya kazi zako vizuri.

Hizi ni njia tatu za kukusaidia kuweza kufanya kazi zako ukiwa nyumbani.

  1. Jenga mazoea ya kufanya kazi maeneo ya wazi kama vile mgahawa. Mara nyingi katika sehemu kama hizo kuna uwezekano mkubwa wa kukutana na wajasiriamali wengine na hivyo itakupa nafasi ya kujifunza baadhi ya vitu vipya. Kufanya kazi nje ya nyumbani pia inaweza kukuhamasisha kufanya kazi zaidi kuliko kukaa nyumbani siku nzima. Ukiwa sehemu kama hizi utaelekeza jitihada zote kwenye kazi na sio kitu kingine.
  2. Jiunge na kundi la ujasiriamali. Unaweza kutafuta kundi la wajasiriamali karibu la eneo ulipo au hata kupitia mitandao ya kijamii kama Facebook na Instagram. Ukweli ni kwamba hakuna anayemuelewa mjasiriamali kama mjasiriamali mwenzake hivyo inakuwa rahisi kubadilishana ushauri na mawazo. Hii huchochea maendeleo kwani watu wanaokuzunguka wanakuhamasisha kuboresha biashara na maisha yako kwa ujumla. Pia kupitia vikundi unaweza kupata wateja wapya na kupanua soko lako.
  3. Zingatia muda. Badala ya kufanya kazi bila mpangilio maalum ni vizuri kuwa na ratiba itakayokuongoza na kupata majukumu yako vizuri. Tenga muda wa kupumzika kama umeapnga kufanya kazi usiku. Kufanya kazi haimaanishi kuwa unatakiwa kufanya kazi siku nzima bila kupumzika. Panga ratiba yenye muda maalum kwa ajili ya mapumziko.

Kufanya kazi kutoka nyumbani kuna changamoto zake na usipokuwa makini unaweza kujikuta unashindwa kufikia malengo yako. Ni muhimu kuwa na mpangilio maalum ili kuhakikisha unafanya kazi na kutimiza malengo yako.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter