Home AJIRA Waziri ataka changamoto ajira za walimu zishughulikiwe

Waziri ataka changamoto ajira za walimu zishughulikiwe

0 comment 149 views

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Innocent Bashungwa amemwagiza Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Elimu, Dkt. Charles Msonde kufuatilia malalamiko na changamoto zote zinazowakabili walimu wa ajira mpya 9,800.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari, Bashungwa amesema amekuwa akipokea malalamiko mengi  kutoka wa walimu wa ajira mpya zilizotolewa na Serikali mwezi Juni, 2022 ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa baadhi ya wilaya ambazo hazijatoa fedha za kujikimu kwa walimu hao.

Aidha, Bashungwa ameagiza kutolewa kwa ufafanuzi wa viwango vya malipo kwa mujibu wa tararibu na vigezo vinavyotumika katika malipo hayo ili kuondoa sintofahamu ambazo zimekuwa zikijitokeza mara kwa mara.

Bashungwa amesema serikali ya awamu ya sita ni sikivu na itaendelea kusikiliza na kutatua changamoto watakazokumbana nazo walimu wakati wakitekeleza majukumu ya kuwafundisha wanafunzi.

Juni 26, 2022 Serikali ilitoa ajira za kada za ualimu kwa waombaji wenye sifa waliokidhi vigezo 9,800 ambapo walimu 5,000 wamepangwa shule za msingi na walimu 4,800  shule za sekondari.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter