Home AJIRA Waziri ataka shirika la utalii duniani kuzingatia usawa utoaji ajira

Waziri ataka shirika la utalii duniani kuzingatia usawa utoaji ajira

0 comment 193 views

Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Jasmine Kairuki ametoa wito kwa Shirika la Utalii Duniani (UNWTO) kuzingatia usawa katika kutoa ajira ikiwemo masuala ya kijinsia.

Wito huo umetolewa Oktoba 16, 2023, wakati akichangia mjadala katika Kikao cha Kamati ya Programu na Bajeti ya Shirika la Utalii Duniani, ambayo Tanzania ni mjumbe anayemaliza muda wake.

Kikao hicho kimefanyika sambamba na Mkutano Mkuu wa 25 wa Shirika la Utalii Duniani jijini Samarkand, Uzbekistan.

Akichangia katika kikao hicho, Kairuki ameelezea utayari wa Tanzania kuendelea kufanya kazi na Shirika la Utalii Duniani hususan kupitia miradi inayotekelezwa na Shirika hilo.

Aidha, Waziri amewashukuru UNWTO na Mradi wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa kuwezesha na kutoa mafunzo ya Kutangaza Utalii kwa njia za Kidigitali kwa Wadau wa Chama cha Wasafirishaji Watalii Tanzania (TATO).

Amepongeza juhudi za mashirika hayo katika kuandaa mkakati utakaounganisha Utalii na maendeleo ya kiuchumi kwa wazawa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter