Home AJIRA Waziri Mkuu apokea taarifa nyongeza ya mishahara

Waziri Mkuu apokea taarifa nyongeza ya mishahara

0 comment 125 views

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea taarifa ya mapendekezo ya ongezeko la mishahara ya watumishi kutoka kwa timu ya wataalamu iliyokuwa ikiyaandaa kwa ajili ya kuiwasilisha kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Amepokea taarifa hiyo Jumanne, Mei 10, 2022 katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma.

Kikao hicho kiliwahusisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba.

Viongozi wengine waliohudhuria kikao hicho ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad Hassan Chande, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi pamoja na Makatibu Wakuu wa wizara hizo.

Waziri Mkuu amesema taarifa hiyo imeonesha kwamba maandalizi ya mapendekezo ya ongezeko la mishahara yameshakamilika na kwamba wakati wowote atayawasilisha kwa Mhe. Rais Samia ambaye atautangazia umma mabadiliko hayo yanayotarajiwa Julai mwaka huu.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia wananchi katika sherehe za maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani Jumapili Mei Mosi 2022 aliwahikikishia wafanyakazi nchini kuwa Serikali katika mwaka wa fedha 2022/2023 itaongeza mishahara kwa watumishi wake.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter