Home BENKI WB yaijaza manoti Tanzania

WB yaijaza manoti Tanzania

0 comment 109 views

Benki ya Dunia (WB) imeipatia Tanzania mkopo wa sh 1.8 trilioni kwa lengo la kutekeleza miradi endelevu vijijini hususani ya maji,mazingira na umeme. Miradi ya maji na mazingira itakuwa katika wilaya 86 huku mradi wa kuendeleza na kuunganisha umeme utakuwa kutoka Zambia kwenda mikoa minne ya kusini mwa Tanzania.

Katika fedha hizo zilizotengwa,Sh 1.04 trilioni zitakuwa kwa ajili ya usambazaji wa umeme huku Sh. 800 billioni zikiwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji na mazingira. Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya utiaji saini kati ya Benki ya Dunia na Tanzania, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James alisema mkopo huo wenye masharti nafuu utasaidia kupunguza tatizo la maji na kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wananchi husika. Mkopo huo pia utasaidia kuongeza uzalishaji wa umeme na upanuzi wa miundombinu ya umeme.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird amesema mkopo huo utasaidia kupunguza magonjwa kama kipindupindu yanayotokana na uchafuzi wa mazingira hasa matumizi ya vyoo visivyo safi na salama kwani watanzania wengi hupendelea kuboresha nyumba zao kuliko vyoo.

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter