Home BIASHARA Air Tanzania kufika Zambia, Zimbabwe

Air Tanzania kufika Zambia, Zimbabwe

0 comment 111 views

Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limetangaza gharama za safari zake kati ya Dar es salaam, Harare (Zimbabwe) na Lusaka (Zambia) ambazo zinatarajiwa kuanza hivi karibuni. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika hilo, nauli ya Lusaka itakuwa Dola 218 za Marekani (Sh. 502,000 za Tanzania) kwa safari moja pekee huku gharama ya kwenda na kurudi ikiwa Dola 374 (Sawa na Sh. 862,000).

Kwa upande wa safari za Harare, nauli itakuwa Dola 214 za Marekani (Sh. 493,000 za kitanzania) kwa safari moja huku safari ya kwenda na kurudi ikigharimu Dola 317 za Marekani, sawa na Sh. 726,000.

Hivi sasa, Shirika la ATCL linafanya safari za kimataifa katika nchi tatu za Uganda, Comoro na Burundi huku ikiwa na ndege sita zinazofanya kazi. Safari za miji hiyo zitafanyika siku za Jumanne, Ijumaa na Jumapili.

Siku chache zilizopita, Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli aliongoza mamia ya watanzania katika mapokezi ya ndege mpya ya Airbus A220-300 iliyotokea nchini Canada ikiwa ni muendelezo wa jitihada zinazofanywa na serikali kufufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) na kuimarisha usafiri wa anga hapa nchini.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter