Home BIASHARA Biashara zinazolipa zaidi Tanzania

Biashara zinazolipa zaidi Tanzania

0 comment 395 views

Biashara ni sekta ambayo imekuwa kimbilio kwa watanzania wengi na hivyo kuifanya kuwa na umuhimu mkubwa katika uchumi wetu. Idadi kubwa ya watu hususani vijana wamekuwa wakiwekeza nguvu zao katika ujasiriamali ili kujiingizia kipato na kujijenga kiuchumi. Hapa nchini, ajira imekuwa changamoto kubwa na ili kujikomboa na kupiga vita umaskini, wengi wamewekeza nguvu kubwa katika biashara.

Kuna wale waliofanikiwa kuwa na mitaji inavyojitosheleza na hivyo kuwa wafanyabiashara wakubwa lakini kundi kubwa la watu ni watanzania wa kawaida wenye mitaji midogo hivyo hata mawazo yao ya biashara ni yale ya kawaida tu. Japokuwa kuna biashara za aina mbalimbali, zinazofuata ni biashara zinazofanywa kwa wingi hapa kwetu.

Biashara ya Chakula. Hii ni biashara kubwa zaidi hapa Tanzania. Ukweli ni kwamba lazima watu wale hivyo watu wengi huwekeza hapa kutokana na uhakika wa soko. Japokuwa kuna ushindani kubwa katika biashara hii, wengi wamefanikiwa kuendesha maisha yao na kufanikiwa kutokana na biashara hii.

Aina nyingine ya biashara inayofanywa kwa wingi ni Urembo na Vipodozi. Mafanikio katika biashara hii yanatokana kwa kiasi kikubwa na kufahamu soko lako vizuri na kujua ni nini hasa wanahitaji. Wanawake ndio soko kubwa katika biashara hii. Ili kuwa katika nafasi nzuri zaidi, mfanyabiashara wa sekta hii anapaswa kuendana na wakati na kujua ni bidhaa gani zinapendelewa zaidi. Mitandao ya kijamii nayo ina mchango mkubwa katika kuhakikisha aina hii ya biashara inafika mbali.

Ukizungumzia sekta ya biashara ni lazima kuzungumzia Biashara ya Nguo. Kama ilivyo chakula, mavazi pia ni moja kati ya hitaji la msingi kwa binadamu. Wajasiriamali wengi wamekuwa wakiwekeza katika nguo kwa kuangalia ni nini hasa jamii inahitaji na kwa wakati gani. Kuna wale waliofungua maduka makubwa ya nguo za ofisini, suti, sherehe, za watoto n.k. pia kuna wale waliojikita katika kuuza nguo za mitumba na kufanikiwa. Jambo la msingi katika biashara ya nguo ni kuhakikisha bei yako ni rafiki kwa jamii na aina ya nguo unayouza ina ubora unaotakiwa. Biashara ya mavazi imeonyesha mafanikio kwa kiasi kikubwa hapa nchini huku watu wengi zaidi wakionyesha nia ya kujiingiza katika biashara hii kila siku.

Simu, kompyuta, vifaa vya kieletkroniki na umeme kwa ujumla nayo ni biashara kubwa hapa kwetu. Hii inatokana na kwamba tunaishi katika ulimwengu wa kisasa na hivyo vifaa kama hivi husaidia kurahisisha kazi na kuokoa muda. Uhitaji wa vifaa hivi unaendelea kukua siku hadi siku kutokana na kasi ya ukuaji wa teknolojia. Matumizi ya vifaa hivi yameendelea kuwa na umuhimu mkubwa katika maisha yetu ya kila siku na hivyo soko lake limebaki kuwa la uhakika.

Ukiachana na biashara hizo hapo juu, aina nyingine ya biashara inayofanya vizuri ni Biashara ya vifaa vya shule. Wanafunzi kwa kawaida huitaji vifaa mbalimbali kama madaftari, kalamu, vitabu n.k hivyo biashara hii mara nyingi huwa na soko la uhakika. Kama unafikiria kuwekeza katika hili ni muhimu sana kuzingatia eneo la kufanyia biashara na kufahamu nini hasa wanafunzi wanahitaji kwa muda huo.

Kuna biashara nyingi ambazo kwa kiasi kikubwa zinavutia watu wengi kufanya hapa nchini. Ili kuendelea kuweka mazingira mazuri katika sekta hii, wafanyabiashara wanapaswa kushirikiana na serikali na kuhakikisha wanafuata taratibu zilizopo kwani kufanya hivyo kutawaruhusu kuendesha shughuli zao kwa amani na uhuru. Serikali nayo inapaswa kuendelea kutatua changamoto mbalimbali zinaziwakabili wafanyabishara ili kuvutia watu wengi zaidi kuendelea kuwekeza katika sekta hii ambayo imeajiri mamia ya watanzania kote nchini.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter