Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limetangaza kusitisha safari za kwenda nchini India ambako vifo na maambukizo ya corona yanazidi kuongezeka.
Taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji mkuu wa shirika hilo, Ladislaus Matindi inasema safari hizo zimesitishwa kuanzia Mei 4.
Taarifa hiyo imewataka abiria wote wenye tiketi za ATCL kuwasiliana na ofisi za ATCL au mawakala wao kwa taratibu za kubadilisha tiketi ili zitumike pindi safari zitakaporejeshwa tena bila gharama yoyote.
Mei 4 pekee, taarifa nchini India zilitoa idadi ya maambukizo mapya 357,229 na kufanya jumla kuwa zaidi ya milioni mbili. Kwa idadi hiyo, India inakuwa miongoni mwa mataifa yenye maambukizo mengi zaidi duniani.