Home KILIMO Pembejeo feki bado changamoto

Pembejeo feki bado changamoto

0 comment 80 views

Wakulima wa kahawa kutoka mikoa ya Arusha na Kilimanjaro wamelalamikia kitendo cha baadhi ya wafanyabiashara wa pembejeo kuingiza sokoni pembejeo feki bila kujali athari zinazotokana na matumizi ya pembejeo hizo. Wakulima hao wametoa malalamiko yao katika mkutano wa wadau wa zao la kahawa uliofanyika mkoani Kilimanjaro, ukiwa na dhumuni la kujadili mikakati ya kufufua na kuendeleza kilimo hicho.

“Idadi kubwa ya wakulima wameachana na kilimo cha kahawa na kuanza kujihusisha na kilimo cha mboga ambacho kinalipa sana, kwa sababu bei ya kahawa imeshuka katika soko dunia. Kwa sasa pembejeo nyingi zinazouzwa katika maduka hazina matokeo mazuri kwa mkulima anapotumia na hasa haya madawa ya kuzuia na kuangamiza wadudu waharibifu wa mazao shambani maarufu kama viuatilifu. Mara nyingi tunapolima hatufikii malengo yetu”. Amesema Godfrey Msela, mmoja kati ya wakulima walioathirika ya uwepo wa pembejeo feki.

Kwa upande wake, Meneja wa mradi kutoka shirika la Solidaridad Tanzania, Mary Mkonyi amesema hivi sasa shirika hilo limeanzisha mchakato maalum wa kupima udongo ili kufahamu rutuba iliyopo mashambani huku wakiunganisha wakulima na mawakala wa pembejeo, pamoja na taasisi za kifedha ili kuinua kilimo hicho na kusaidia wakulima kuepuka hasara inayotokana na kutumia pembejeo zisizo na viwango.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter