Mkuu wa Wilaya ya Mbarali jijini Mbeya, Reuben Mfune ametoa muda wa siku kumi kwa wafanyabiashara wadogo kuhakikisha wanapata vitambulisho vilivyotolewa na Rais Magufuli. Mfune ametoa agizo hilo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali kilicholenga kupitisha muhtasari wa mpango na bajeti ya miaka mitatu pamoja na makadirio ya mapato kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
“Kufikia tarehe 10 mwezi Februari kila machinga awe na kitambulisho, nia ni njema kwamba tunahitaji kuwatambua, lakini kuongeza mapato kwa serikali yetu wala ambao wana namba ya utambulisho yaani Tin, lakini sio za kibiashara pia wanatakiwa kupewa vitambulisho waliochukua namba hizo kwa ajili ya biashara hawapaswi kupewa, jambo hili ni la haraka na dharura watendaji wote wa kata, makatibu tarafa mnayo kazi ya kuwahamasisha machinga kuvichukua”. Ameeleza Mkuu huyo wa wilaya.