• Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
Sunday, February 5, 2023
  • Login
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
No Result
View All Result

Tanzania, Kenya zasaini mkataba wa mauzo korosho ghafi

Patricia Richard by Patricia Richard
January 31, 2019
in HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI
0
Tanzania na Kenya zasaini mkataba wa korosho ghafi

Viongozi mbalimbali wakishuhudia zoezi la utiaji saini mkataba wa mauzo ya korosho ghafi tani laki moja kwa Kampuni ya ENDO Power Solutions ya Kenya.

Share on FacebookShare on Twitter

Serikali kupitia Bodi ya Taifa ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko imesaini mkataba wa mauzo ya korosho ghafi tani laki moja kwa Kampuni ya ENDO Power Solutions ya Kenya kwa Sh. 418 bilioni. Mkataba huo umesainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo, Dk. Hussein Mansoor kwa niaba ya serikali ya Tanzania na kwa upande wa Kenya, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ENDO Power Solutions, Brian Mutembei amesaini makubaliano hayo.

Baadhi ya viongozi walioshuhudia zoezi hilo ni Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda, Naibu Waziri wa Kilimo, Dk. Innocent Bashungwa, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. Florence Luoga. Wengine ni Balozi wa Kenya hapa nchini, Dan Kazungu, Prof. Sifuni Mchome, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Joseph Buchweshaija, Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara, Prof. Siza Tumbo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Edwin Rutaberuka, Mkurugenzi wa TanTrade, maafisa kutoka serikalini pamoja na waandishi wa habari.

Akizungumzia hatua hiyo, Prof. Kabudi amempongeza Rais Magufuli kwa uamuzi wa serikali kununua korosho yote na kuwawezesha wakulima kupata bei inayolingana na jasho lao. Aidha, Waziri Kakunda amewataka watanzania na wamiliki wa viwanda kutokuwa na wasiwasi kwani serikali inalenga kuleta maendeleo kwa wananchi hasa kupitia sekta ya kilimo cha korosho.

ADVERTISEMENT

“Wakulima wa Korosho wanatakiwa kumshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa uamuzi wake ambao unalinda maslahi ya mkulima na umewawezesha kuuza korosho zao kwa faida. Nawakaribisha wafanyabiasha makini kuja nchini kwani Serikali ipo tayari kuwasikiliza watu wa aina hiyo na kufanya nao biashara”. Amesema Kakunda.

Mkataba huo umesainiwa wakati baadhi viongozi hapa nchini wakiwa jijini Arusha kwa ajili ya kuhudhuria vikao vya maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).

Tags: ENDO Power SolutionsKenyakoroshoMagufuliviwanda
Patricia Richard

Patricia Richard

Next Post
Kinachopelekea biashara nyingi kutoendelea

DC Mbeya asisitiza machinga kuchangamkia vitambulisho

Discussion about this post

Habari Mpya

Baadhi ya vijana wakiwa kwenye Kongamano la Vijana wa Vyuo Vikuu na Vyuo vya Kati lijulikanalo kama ‘University Ladies and Gentlemen Conference.

Vijana wahamasishwa kuchangamkia fursa za kilimo

January 31, 2023
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Angellah Kairuki.

Halmashauri Tanzania zakusanya 485.42 bilioni

January 31, 2023
Mohammed Dewji (Mo Dewji). Picha|Mtandao

Watieni nguvu wawekezaji: Makalla

January 30, 2023

Vijana Tanzania kupatiwa eka 10 kulima

January 30, 2023

Poland kuisaidia Tanzania kuweka mifumo ya kodi kidigitali

January 26, 2023

Kamati ya bunge yahimiza uwekezaji maeneo ya hifadhi

January 21, 2023

KUHUSU SISI

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905. PesaTu inamlenga kila mtu ambaye kwa namna moja au nyingine anaguswa na anapenda kujua/ kufuatilia masuala mbalimbali ya kiuchumi ya nchi ikiwemo ujasiriamali, uwekezaji, viwanda, kilimo na hisa.

LATEST

Baadhi ya vijana wakiwa kwenye Kongamano la Vijana wa Vyuo Vikuu na Vyuo vya Kati lijulikanalo kama ‘University Ladies and Gentlemen Conference.

Vijana wahamasishwa kuchangamkia fursa za kilimo

by Pesatu Reporter
January 31, 2023
0

Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde amewataka vijana nchini Tanzania kuchangamkia fursa zilizopo kwenye sekta ya kilimo kupitia utekelezaji wa...

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Angellah Kairuki.

Halmashauri Tanzania zakusanya 485.42 bilioni

by Pesatu Reporter
January 31, 2023
0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Angellah Kairuki amesema kipindi cha mwezi July...

RECOMMENDED

Waziri Mwijange aja na orodha ya viwanda visivyofanya kazi

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

  Na Mwandishi wetu. Baada ya Rais John Magufuli kuonyesha kukerwa na kitendo cha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji...

Nane Nane itumike kama darasa huru kwa wakulima

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

Na Mwandishi wetu Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imejitolea kuwapa mafunzo ya siku moja wakulima mkoani Lindi...

No Result
View All Result
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI

© 2023 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In