Home BIASHARA DStv yatangaza promosheni ‘Panda Tukupandishe’

DStv yatangaza promosheni ‘Panda Tukupandishe’

0 comment 104 views

‘Panda Tukupandishe’ promosheni iliyotangazwa na kampuni ya Multichoice Tanzania maalumu kwa wateja wa DStv ambapo kwa kipindi cha miezi mitatu itakuwa ikiwapandisha vifurushi wateja wake.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo amesema promosheni hii itawawezesha wateja wa DStv wanaokidhi vigezo yaani wateja ambao akaunti zao zimekatika, wanaoendelea pamoja na wateja wapya.

Amesema wateja watapata fursa ya kulipia kifurushi kinachofatia cha juu yake na kupandishwa kwa kupatiwa kifurushi cha juu ya kile alicholipia kwa muda maalum ambapo inategemea na kifurushi ambacho mteja alikuwa amelipia hadi kufikia Januari 8, 2021.

“Promosheni hii ipo namna hii, mfano mteja wa kifurushi cha Bomba, akilipia kifurushi cha Family atapandishwa hadi kifurushi cha Compact bila malipo ya ziada kwa mwezi mmoja,” amesema.

Amesema kampuni hiyo inaendelea kuwapa wateja wake burudani ya kina bila kusahau maudhui mengine kama habari na elimu na kuhakikisha wateja wake wanapata maudhui kemkem ya kusisimua ya ndani na nje ya nchi.

Nae Kaimu Meneja wa Thamani kwa Wateja Lucy Kisasa alifafanua kuwa wateja wa DStv ambao wamelipia kifurushi kwa mwaka mzima hawahusiki na promosheni hii kwa kuwa wao tayari wana ofa yao ambapo hupata mwezi mmoja wa kifurushi bila malipo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter