1.Una uhakika wa kipato cha kuendesha maisha
Unapokua katika ajira inamaanisha kwamba utakua unapata mshahara,hivyo basi kutokana na kipato utakachokua unaingiza kila pindi unapokea mshahara unaweza ukatenga asilimia kadhaa kwa ajili ya kufanya/kuanza biashara.Ni rahisi kuanzisha biashara nyingine pembeni itakayokua inakuongezea kipato.
2.Unaweza kukusanya mtaji kutoka kwenye mshahara wako.
Kwa kua tayari upo katika ajira na una uhakika wa kupokea mshahara,basi ni rahisi kuanzisha biashara kwa kutumia mshahara wako mwenyewe kama mtaji wa kuanzisha biashara yako.Tenga kiasi kila mwezi au kwa muda unaofikiri kua utakua umetunza pesa za kutosha mtaji wa biashara unayotaka kuianzisha.
3.Unaweza kutumia kazi yako kukutana na wateja wa biashara yako.
Unapokua kazini kwako ni rahisi kukutana na wateja watakaonunua bidhaa zako,maana ni sehemu unaweza hata ukatengeneza njia rahisi ya malipo baina yako wewe na wafanyakazi wenzako ambao ndio watakua wateja wako,pia watu wa karibu na eneo lako la kazi.Urahisi mwingine ni kuweza kuongeza wateja kwa kupitia wafanyakazi wenzako,kwa kukutangazia biashara yako kama tu biashara yako itakua ina wavutia na kuwapendeza wao kwanza
4.Huhitaji kuitegemea biashara mapema na hivyo kuipa nafasi ya kukua.
Kwa kawaida biashara huitaji muda ili kuanza kutengeza faida,hivyo basi unapokua una ajira kutakusaidia kutokana na kua tayari una njia nyingine ya kukuingizia kipato bila kutegemea biashara yako,hivyo utaifanya ikue na kuweza kujiendesha pia kukuingizia faida lukuki.
5.Unaweza kujaribu vitu tofauti tofauti mpaka upate unachopenda.
Kwa kua tayari upo katika ajira,inakufanya usiwe tegemezi wa kutaka kupata pesa itokanayo na biashara haraka haraka,hivyo basi kwa kua unakua unakua unainakupa uwanja mpana wa kujaribu vitu tofauti,ili tu uweze kufikisha malengo yako na kupata biashara unayoona kua unaweza kuimudu pia changamoto zake
Hizo ni baadhi ya njia ambazo zinaweza kukuongezea kipato pale tu unapoamua kuanza biashara wakati upo katika ajira.