Home BIASHARA JPM awafurahisha wafanyabiashara wa Oman

JPM awafurahisha wafanyabiashara wa Oman

0 comment 133 views

Mwenyekiti wa Baraza la Biashara kati ya Tanzania na Oman Sheikh Saud Al Rawahi amesema wafanyabiashara kutoka Oman wamefurahishwa na hatua ya serikali ya Tanzania chini ya Rais Magufuli kununua ndege mpya na kushauri serikali kununua ndege ya mizigo ili kurahisisha biashara kati ya mataifa hayo mawili.

Sheikh Al Rawahi amesema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kibiashara kati ya Oman na Tanzania ambapo wafanyabiashara wa nchi hizo mbili walipata fursa ya kujadili masuala mbalimbali ya kibiashara. Mwenyekiti huyo ameeleza kuwa, jitihada zinazofanywa na Rais Magufuli mbali na kuinua uchumi wa taifa pia ni hatua kubwa katika kuimarisha sekta ya anga.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhani Mwinyi amewashauri wafanyabiashara wa hapa nchini kuchangamkia fursa na kupeleka bidhaa zao nchini Oman kwani kwa mujibu wa takwimu, bidhaa zinazouzwa hapa nchini kutoka Oman ni nyingi kuliko za Tanzania zinazouzwa nchini Oman. Mwinyi amewataka wafanyabiashara kutumia fursa hiyo na kupeleka bidhaa zaidi katika taifa hilo.

Naye Balozi wa Tanzania nchini Oman, Abdalah Kilima amesema takribani asilimia 90 hutegemea bidhaa kutoka nje ya nchi hivyo ni nafasi nzuri kwa watanzania kuuza bidhaa zao nchii Oman.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter