Home KILIMO Tizeba awaonya walima kahawa wanaokimbia Uganda

Tizeba awaonya walima kahawa wanaokimbia Uganda

0 comment 42 views

Waziri wa Kilimo Dk. Charles Tizeba amewataka wakulima wa kahawa mkoani Kagera kupuuza taarifa kuwa, kuna soko zuri la bidhaa hiyo nchini Uganda kwani bei ya huko ni sawa na ile ya hapa nyumbani. Dk. Tizeba amefafanua kuwa, taarifa za bei kuwa nzuri zaidi nchini Uganda sio za kweli huku kitaja sababu ya baadhi ya watu kwenda huko kuwa ni mikopo isiyo rasmi wanayokopeshana (Butura).

Kwa mujibu wa taarifa za bei ya kahawa kutoka soko la Uganda, kilo moja ya bidhaa hiyo yenye maganda inagharimu kiasi cha Sh. 2000 ambayo ni sawa na Sh. 1400 za kitanzania wakati kwa hapa nyumbani, kilo moja ya kahawa hugharimu Sh. 1460 kwa bei elekezi.

Kwa upande wake, Waziri wa Biashara na Ushirika kutoka nchini Uganda Fredrick Gume amehakikisha kwa Waziri Tizeba kuwa, nchi yake inakumbana na changamoto kama za Tanzania, kutokana na mikopo isiyo rasmi wanayochukua wakulima kuwa katika kiwango cha juu.

Mawaziri hao wawili walikutana na kufanya mazungumzo muda mchache uliopita ambapo Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage nae alipata nafasi ya kuhudhuria na kuzungumza nao. Mkutano huo ulifanyika kufuatia agizo la Rais John Magufuli la kuitaka Wizara ya Kilimo kufuatilia sababu zinazopelekea wakulima wa kahawa wanakimbilia nchini Uganda pamoja na kufahamu kinachopelekea malipo ya wakulima hao kuchelewa.

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter