Home BIASHARA Kariakoo saa 24

Kariakoo saa 24

0 comment 174 views

Mara baada ya ujenzi wa soko la Kariakoo kukamilika biashara zinatarajiwa kufanyika kwa saa 24.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla ameeleza hayo Julai 18, 2022 alipokutana na watendaji na viongozi wa mkoa kuzungumzia kampeni yake ya kuiependezesha Dar es Salaam.

Mkuu huyo wa mkoa amesema Dar es Salaam ni Jiji la biashara haoni ni sababu gani watu walale na kikubwa ni kutengeneza mazingira ili utekelezaji wa kufanya biashara saa 24 ufanyike.

“Tunakoelekea hata kabla ya soko halijaisha lakini tukajiridhisha mazingira yanaruhusu, Dar biashara itakuwa saa 24 na soko likiisha ndio kabisaa.

“Tunataka mtu anatoka Zambia anafika leo anafanya manununuzi yake muda wowote anaotaka na kuondoka,” amesema Makalla.

Amesema ili kufanikisha hilo, kuna mpango wa kufunga taa kila eneo la Jiji hilo ambapo hakutajulikana ni mchana au usiku.

Soma Zaidi: Bilioni 28 kujenga Kariakoo mpya

 

Julai 10, 2021 soko hilo la kimataifa liliteketea kwa moto.

Katika tukio hilo, Rais Samia Suluhu Hassan aliviagiza vyombo vya Ulinzi na Usalama kufanya uchunguzi wa kina kujua chanzo cha moto.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliunda Kamati maalumu kwa ajili ya kuchunguza ajali ya moto huo.

Waziri Mkuu pia alitoa agizo kwa benki na taasisi za fedha kuangalia namna ya kuwaongezea muda wa kurejesha mikopo wafanyabiashara walioathirika na katika tukio hilo.

Julai 27, 2021 Majaliwa alipokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati CP Liberatus Sabas na kuahidi kuwa Serikali itayafanyia kazi mapendekezo yote yaliyotolewa.

Vilio vya wafanyabiashara masoko kuungua moto

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter