Home VIWANDANISHATI Vituo 5 vya gesi asilia kujengwa nchini

Vituo 5 vya gesi asilia kujengwa nchini

0 comment 34 views

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kufikia Desemba, 2023, linatarajia kujenga vituo vitano vya gesi asilia nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonyesho ya 16 Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dk. James Mataragio amesema vituo hivyo vitasaidia kupunguza malalamiko ya kuwa na vituo vichache vya gesi asilia.

Amesema mpaka sasa TPDC imegundua kiasi cha gesi futi za ujazo Trillion 57.54.

Dk. Mataragio ameeleza kuwa “kiasi kikubwa cha gesi kipo baharini, tunatarajia kukivuna, kwasasa tunaendelea na mtambo wa Liquefied Natural Gas (LNG) ambao utachakata gesi hiyo.

Amefafanua zaidi kuwa baada ya kuchakatwa gesi itapoozwa hadi kufikia juzi joto 160 ambapo itasafirishwa kwenda kwenye masoko ya nje huku kiasi kitakachobaki kitatumika kwa ajili ya soko la ndani.

Ameeleza kuwa matumizi makubwa ya gesi asilia ni kuzalisha umeme ambapo gesi inachangia asilimia 62 kwenye gridi ya taifa huku asilimia 20 ya gesi imekuwa ikitumika kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na viwandani ambapo magari yanatumia gesi ya Compressed Natural Gas (CNG).

Amesema “mteja atakuwa anaenda kwenye vituo vyetu ili kuweza kuweka gesi kulingana na uhitaji wake”.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter