Home BIASHARA Kilimo kitakuza biashara-Samia

Kilimo kitakuza biashara-Samia

0 comment 154 views

Makamu wa raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mh.Samia Suluhu Hassan amesema biashara baina ya Tanzania na Malawi itakua na kuongezeka endapo mkazo utatiliwa zaidi katika kuboresha kilimo na kuanzishwa kwa viwanda vidogo vidogo vya kuongeza thamani ya mazao.

Aliyasema hayo jana wakati akifungua kongamano la biashara na uwekezaji baina ya nchi hizo mbili ambapo wafanyabiashara wakubwa na wadogo kutoka nchi zote walikutana na kubadilishana mawazo.

Samia alisisitiza uwekaji mkazo katika sekta ya kilimo ni muhimu katika kuongeza thamani ya biashara na uzalishaji wa bidhaa viwandani,pia alisisitiza kuhusu kudumisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili hasa ule wa kibiashara.

“kongamano hili ni mwanzo mzuri wa kujenga ushirikiano ulio imara katika kukuza uchumi”,alisema samia.

Kongamani hilo lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwamo mkuu wa mkoa wa mbeya mh.Amos Makala pamoja na mbunge wa mbeya mjini mh.Joseph Mbilinyi huku kwa upande wa Malawi ukiwakilishwa na waziri wa viwanda,biashara na utalii wa nchi hiyo mh.Henry Mussa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter