Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Edwin Rutageruka amesema nchi 29 zimedhibitisha kushiriki maonyesho ya 42 ya kimataifa ya sabasaba yanayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu.
Rutageruka ameeleza kuwa baadhi ya nchi zitakazoshiriki maonyesho hayo ni pamoja na China, Nigeria, Malawi, Japan, Malaysia na Afrika Kusini. Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa maonyesho ya sabasaba yatafanyika kwa siku 16 kuanzia Juni 28 mpaka Julai 13 na mpaka sasa,takribani kampuni 2,456 za ndani tayari zimedhibitisha kushiriki huku taasisi 120 kutoka serikalini nazo zikidhibithisha uwepo wake katika maonyesho hayo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa huduma wa TanTrade Martha Paul ametoa wito kwa wafanyabiashara kukodi maeneo kufanya hivyo mapema ili kuepuka usumbufu baadae kwani tayari asilimia 89.4 ya majengo tayari yameshakodiwa hadi sasa.