Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan amekabidhi cheti na tuzo kwa Meneja Biashara na Mkakati wa Mauzo wa Vodacom Tanzania kanda ya Pwani, Caleb Majo, kwa kutambua udhamini walioutoa katika kipindi hiki cha maonesho ya 43 ya sabasaba 2019, jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Cheti na Tuzo Meneja Biashara na Mkakati wa Mauzo wa Vodacom Tanzania kanda ya Pwani, Caleb Majo, kwa kutambua udhamini walioutoa katika kipindi hiki cha maonesho ya 43 ya sabasaba 2019, jijini Dar es Salaam jana. Kwa miaka mingi Vodacom Tanzania imekuwa ikidhamini maonyesho ya sabasaba upande wa mawasiliano na mwaka huu wamewaandalia wateja wao huduma za kidijitali katika banda lao kwenye maonyesho hayo yanayoendelea.