Home BIASHARA Mambo ya kuzingatia kuhusu eneo la biashara

Mambo ya kuzingatia kuhusu eneo la biashara

0 comment 119 views

Maamuzi kuhusu eneo la biashara yanaweza kuleta matokeo mazuri au mabaya katika biashara. Kabla hujaanza kutafuta eneo unatakiwa kuwa na picha kamili ya kile unachokitaka kwa muda huo na siku zijazo. Kuwa na picha kamili kutakusaidia kutumia muda mchache katika utafutaji wa eneo.

Ingawa makosa mengi yanaweza kurekebishwa baada ya kuanzisha biashara lakini suala la eneo si rahisi kurekebisha kwa haraka. Hivyo zingatia haya kupata eneo sahihi la biashara:

Mtindo wa uendeshaji wa  biashara yako ni moja ya masuala muhimu wakati unatafuta eneo la biashara. Unatakiwa kujiuliza je biashara yako itakuwa inaendeshwa katika mfumo rasmi, wa kifahari au kawaida? Na kama unataka kuuza bidhaa za rejareja je kuna umuhimu wa kutafuta fremu au kuuza bidhaa zako mtandaoni?

Wakati unataka kutafuta eneo la biashara wafikirie wateja, urahisi wa kufika eneo la biashara hasa kwa watu wanaotembea kwa miguu utasaidia biashara kupata wateja wengi zaidi. Hivyo fanya utafiti wa kutosha kuhusu eneo linalohitaji bidhaa au huduma unayotaka kuanzisha kisha fanya mpango wa kupata eneo katika mazingira husika.

Pia ni muhimu kuzingatia maegesho ya magari (parking), si kila mtu anayefika katika biashara yako anatembea kwa miguu hivyo ni muhimu kuwafikiria watu wenye magari, watu wenye ulemavu, wazee nk.

Vilevile zingatia biashara zilizopo karibu yako na washindani wako. Jitahidi kutafuta sehemu inayoendana na bidhaa au huduma unayotaka kuanzisha. Kwa mfano ni sawa ukianzisha duka la rejareja karibu na maduka ya kutoa fedha.

Aidha ni muhimu kujua historia ya eneo unalochagua kufungua biashara yako. Fanya utafiti na uliza maswali kuhusu biashara zilizopita na sababu iliyopelekea kufungwa kwa biashara hizo. Kwa sababu historia ya eneo inaweza kuwahamasisha wateja kufika katika biashara yako au kutofika.

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter