Wafanyabiashara sasa wanaweza kuanza kutuma maombi kwa ajili ya kufanya biashara katika kituo kikuu cha mabasi Mbezi Luis ambacho kitaanza kutumika rasmi Novemba 30.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Aboubakari Kunenge amesema ujenzi wa kituo hicho umekamilika kwa asilimia 90.
Wafanyabiashara watakaohitaji kufungua maduka katika shopping mall iliyopo kituoni hapo watatakiwa kutuma maombi kwa njia ya mtandao kupitia TAMISEMI.
Mama lishe, baba lishe na machinga watatakiwa kuandika barua na kupata utambulisho kwa Mtendaji wa Mtaa na kuzipeleka ofisi ya mkurugenzi wa jiji.
RC ametoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa zinazopatikana katika stendi hiyo ikiwemo migahawa, maduka ya fedha, fremu za maduka na zingine nyingi.
Zoezi la kutuma maombi limeanza Novemba 09 hadi Novemba 25.