Home FEDHAMIKOPO MCB kutoa mikopo elimu ya juu

MCB kutoa mikopo elimu ya juu

0 comment 77 views

Benki ya Walimu (MCB) ikishirikiana na Shirika la Global Education Link (GEL), wameanzisha utoaji mikopo elimu ya juu kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya nje ya nchi. Akizungumza katika utoaji wa mikopo hiyo, Mkurugenzi wa GEL,Abdulmalik Mollel alisema mikopo hiyo inatolewa bila riba ili kuwasaidia vijana hao kujiendeleza bila shida yoyote ile.

“ Watu wanajiuliza inawezekanaje kukopa bila riba? Kwa ulimwengu wa sasa inawezekana. Kwa sababu cyuo vitalipa gharama ya mkopo huo ikiwamo riba” Alisema Mollel na kuongeza “Mzazi atalipa asilimia 50 ya ada, benki italipa asilimia 50 ya ada, benki italipa asilimia 50 na vyuo vitalipa gharama za mkopo”

Alivitaka vyuo vya ndani kuchangamkia fursa hiyo ili kuisaidia serikali katika utoaji elimu ya juu.

“Vyuo vikuu vya ndani vijue mzazi akileta mtoto wake kwenye vyuo vyao ni fursa. Watumie wadau hawa kuwawezesha wanafunzi kupata elimu” Alisema Mollel.

Naye Ofisa Mtendaji wa MCB, Ronald Manongi alidai kuwa kama benki wana jukumu la kuhakikisha elimu elimu inaimarika nchini ndiyo maana wamejitosa kwenye utoaji elimu ya Juu.

“Kwa sasa tumeanza na wanafunzi wanaosoma nje, lakini tutakuwa tayari kutoa pia mikopo ya ndani tukishaweka makubaliano” Alisema.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Ofisa Elimu mkoa wa Dar es salaam, Khamis Lissu alisema hatua hiyo ni mafanikio ya utekelezaji wa sera ya Tanzania ya viwanda.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter