Home BIASHARA Mpango wa mafanikio: Jinsi ya kukuza biashara ndogo na za kati (SME’s)

Mpango wa mafanikio: Jinsi ya kukuza biashara ndogo na za kati (SME’s)

0 comment 206 views

IMEANDIKWA NA FARHA MOHAMED, MKUU WA KITENGO CHA BIASHARA, BENKI YA STANBIC NA KUTAFSIRIWA NA LEAH NYUDIKE, PESATU.

Kwa miaka mingi Afrika imekuwa ikitajwa kuwa sehemu ya chanzo cha uchumi wa baadae, kutokana na kuwa na rasilimali nyingi za kiasili na kibinadamu ambazo bado hazijatumika.

Kwa mujibu wa utafiti wa  Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania ina watu milioni 54, hali ambayo imeleta mabadiliko makubwa katika mazingira ya biashara kwa miaka mingi na hivyo  kusababisha biashara ndogo ndogo kukua na kufanikiwa. Licha ya uwepo wa teknolojia na uwezo wa kupata maarifa kwa urahisi bado biashara ndogo ndogo nyingi zimekufa baada ya kuanzishwa kwa kipindi cha muda mfupi.

Ili biashara iweze kupata mafanikio, inahitaji kufanyiwa mabadaliko ya mara kwa mara kulingana na mwenendo wa soko kwa wakati huo, kutilia mkazo mambo yanayofanya kazi iendelee na kuachana na yale yanayokwamisha maendeleo ya biashara. Washauri wa kifedha wanasema misingi ifuatayo itasaidia biashara yako kuwa na mafanikio.

Kuwa na Busara

Malengo ni hatua ya mwanzo ya kila hadithi ya mafanikio,kuwa na mtizamo wa wazi kuhusu wapi unataka biashara yako iwe imefikia baada ya miezi sita, mwaka au hata miaka kumi ijayo. Kuwa na maono ya muda mrefu kutakusaidia kufatilia utendaji wa biashara yako. Masomo ya awali ya biashara yanatusaidia kuwa na malengo ‘smati’ au yanayoeleweka. Mipango yote ya baadae lazima iwe maalum, inayowezekana,inayoweza kutekelezwa, yenye mahusiano na hali halisi, na yanayoweza kufanywa kwa muda muafaka. Ukaguzi wa kawaida wa kifedha utasaidia operesheni za biashara yako ziende vizuri. Huku ukaguzi wa kila mwaka  ni njia bora ya kuhakikisha hali ya biashara yako kifedha  na kuhakikisha kwamba taarifa zako ziko sahihi. Taarifa imara husaidia pale unapotaka kuomba mkopo ili uweze kukuza biashara yako na hivyo kukusaidia katika suala la riba.

Fedha

Wamiliki wengi wa biashara ndogo na za kati hushika majukumu mengi ikiwa ni pamoja na kushughulikia masuala yote katika biashara zao jambo ambalo muda mwingine linawapa hofu hasa katika suala la kuhifadhi fedha. Mara nyingi wafanyabiashara hukata tamaa kutokana na  taratibu  za maombi kuwa ngumu na potofu na hivyo kuwataka kutoa nyaraka nyingi za maandishi. Mtu anaweza kuelekea kwenye mzunguko wa fedha kwa kutafuta benki iliyojikita katika ushauri kwa wafanyabiashara wadogo na yenye nyenzo za kusaidia biashara ndogo na zile za kati. Pia kuwa na historia ya kufanya miamala benki ni moja ya sababu zinazoweza msaidia mtu kupata mkopo. Kama mmiliki wa biashara unatakiwa kuwa na mazoea ya kuwekeza mauzo yako benki ili shughuli zako za fedha zinazohusu biashara ziwe zinaonekana kwenye taarifa ya benki husika. Maombi ya benki kwa kupitia simu ya mkononi hurahisisha miamala ya kila siku. Fedha za muda mfupi na mrefu zitachangia katika historia ya mahusiano kati ya mfanyabiashara na benki. Uwezo wa kukopa ni jambo la thamani sana kwa mmiliki wa biashara ndogo na ya kati.

Kumbukumbu

Kipengele muhimu kinachotofautisha biashara kubwa na ndogo ni kitabu chao cha kumbukumbu. Uchunguzi wa kina kuhusu rekodi za kifedha utakaofanywa na mkaguzi wa kujitegemea  kuhusu kumbukumbu za kampuni yako utaonyesha usahihi wa taarifa  pale utakapohitaji kupata fedha zaidi. Kwa biashara inayokua ni rahisi kujipatia mkopo. Kupitia kumbukumbu inakusaidia kupanga mipango mapema na kuweka kila kitu sawa kama kuna mambo yaanayohitaji tathmini ya mali,uthibitishaji wa uhamisho wa ufanisi  na huduma pamoja na vitu vya kisheria ambavyo vinapaswa kufanyiwa kazi kabla ya kufikia benki kwa ajili ya ufadhili. Kupangilia nyaraka zote kutarahisisha mchakato mzima na kuokoa muda.

Maarifa ni Nguvu

Tathmini biashara yako na sekta inayohusika na biashara hiyo. Kuna habari nyingi mtandao zinazohusu biashara zinazoendana na ya kwako jinsi zilivyoanza kukua na hadi  kufanikiwa. Pia fuata ushauri wa wataalamu kuhusu jinsi ya kuimalisha operesheni ya biashara. Huduma za ushauri ni  kipengele muhimu kwa viwanda vidogo na vya kati ili kufungua uwezo  wa biashara zao kuvuka mipaka zaidi na mipaka ya ugavi mpya. Huduma  hizo zinaweza kupatikana katika mabenki kama Stanbic Tanzania ambayo hutoa  huduma zao moja kwa moja za biashara zikiwalenga SMEs  na huwaunganisha wamiliki wa biashara kwa washauri wa kifedha ili kuzingatia uhalisi wa maswala ya kibiashara  na jinsi ya kukua kibiashara.

Kutoka kwenye kubahatisha hadi kutimiza malengo

Wabahatishaji huwepo kwenye biashara kwa ajili ya kupata faida ya muda mfupi,ili biashara iweze kukua wamiliki wanatakiwa kuachana na mawazo kama haya. Biashara ndogo na za kati huanza kama makampuni madogo kwa ajili ya kujipatia kipato lakini kama hutotengeneza mazingira ya utajiri wa muda mrefu basi biashara yako itakua ikifanya operesheni zake kwa kubahatisha. Biashara ndogo na za kati leo ni mashirika makubwa ya kesho hivyo akili inayowaza mafanikio ya muda mrefu itasaidia jambo hilo kufanyika. Njia ya kufanya kazi kwa biashara ndogo ndogo kwa kutumia njia za kidigitari kwa benki na kuhamisha mapato ya kila siku kutasaidia huko mbeleni.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter