Waziri wa mifugo na uvuvi Mh.Luhaga Mpina leo atatembelea soko la samaki la magogoni ferry kuzungumza na wavuvi kuhusu changamoto na madai yao mbalimbali hasa suala la nyavu sahihi za kutumia kuvulia.
Hayo yalibainishwa na mkuu wa wilaya ya ilala Sofia Mjema ambaye alitembelea maeneo hayo maarufu jijini Dar es salaam kwa kupatikana samaki mbalimbali kujionea shughuli mbalimbali za uvuvi pamoja na kusikiliza kero zinazowakabili wavuvi hao.
Ikumbukwe jana wakati wa fungamano la vyama vya sekta ya uvuvi ukanda wa pwani ya Tanzania ilitangaza rasmi kuhusu kusitishwa kwa shughuli za uvuvi kwa madai ya kuonewa kwa wavuvi hadi mmoja kuuawa huku wengine wakijeruhiwa.