Home BIASHARA Fanya hivi kuvutia wateja

Fanya hivi kuvutia wateja

0 comments 170 views

Mteja akija katika biashara yako, huwa anategemea kupata huduma iliyomleta na kuondoka akiwa ameridhika. Hivyo ili kujitengenezea sifa nzuri kwa mteja ni muhimu kuzingatia tokea anafika hadi anapoondoka katika biashara au kampuni akiwa na furaha.

Mambo ya kuzingatia:

Mafunzo kwa wafanyakazi

Ni muhimu kwa kila mfanyakazi katika biashara yako kutambua kuwa mteja ni mfalme, hivyo anahitaji kuzingatiwa muda wowote na kupewa huduma anayostahili. Hivyo ikiwa mteja anaonekana hajapata huduma mfanyakazi yeyote awe na uwezo wa kumuuliza mteja nini anahitaji kusaidiwa, ikiwa mfanyakazi husika ana uwezo wa kutoa huduma hiyo basi afanye hivyo na ikiwa hawezi basi anaweza kumuelekeza mteja nini cha kufanya, lengo likiwa kutimiza mahitaji ya mteja na kuondoka akiwa ameridhika.

Usafi

Siku zote mteja hujiskia vizuri akienda kununua bidhaa au kupata huduma katika eneo safi. Hivyo ni muhimu kuhakikisha ofisi yako au eneo la biashara yako ni safi muda wote, hii itawavutia watu wengi kuja kukuungisha bidhaa au huduma yako, kinyume na hapo unaweza kukosa wateja wengi kwa sababu ya mazingira machafu.

Ukarimu

Kuna wateja ambao hawana subira. Ikiwa wamefika katika ofisi yako na kukuta mtu wa mapokezi haeleweki au ana lugha mbaya basi wataahirisha kilichowaleta katika eneo lako na kwenda kutafuta huduma hiyo hiyo kwa watu wengine. Hivyo ni muhimu kwa mtu wa mapokezi kuwa nadhifu, mkarimu, mwenye lugha nzuri hata kama muda mwingine atakuwa na kazi nyingi, mteja ni mfalme.

Viburudisho mapokezi

Katika hili haijarishi kama kampuni au biashara yako ni ndogo au kubwa. Mteja akija katika eneo lako la biashara anatakiwa kujisikia vizuri, huku akiwa anasubiri kuhudumiwa. Hivyo inategemeana na muda ambao wateja wanatakiwa kusubiria. Hivyo basi unaweza kuwawekea viburudisho ambavyo vitawafanya wasijisikie upweke wakiwa wanasubiria kuhudumiwa, kwa mfano unaweza kuweka vitabu, au magazeti.

Vielelezo kuhusu kampuni

Ni muhimu kuweka vielelezo kuhusu bidhaa au huduma inayopatikana ili mteja ajue kabisa kama anaweza kupata anachokitaka au la. Kwa mfano unaweza kuweka tangazo kuhusu mipango ya kufanya mkutano mbeleni, unaweza kuweka nyaraka inayoelezea biashara ilipotoka na inakoelekea sehemu ya mapokezi. Hii itamsaidia mteja kupata taarifa kwa ufupi kuhusu ofisi husika.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!