Home BIASHARA ONGEZA KIPATO CHA BIASHARA YAKO KWA KUZINGATIA HAYA

ONGEZA KIPATO CHA BIASHARA YAKO KWA KUZINGATIA HAYA

0 comment 109 views

Kuna umuhimu wa wamiliki wa bidhaa au huduma kuzingatia mikakati ya mauzo ili kuweza kufanikisha mchakato mzima wa utafutaji wa masoko, uuzaji bidhaa na maendeleo ya biashara kwa ujumla.

Hii ni baadhi ya mikakati ambayo kila mfanyabiashara/mtafuta masoko anatakiwa kujua. Ingawa sio kila mkakati utakaotajwa hapa chini unaweza kutumika katika kila biashara lakini kujua mikakati hii kutarahisisha utengenezaji wa mfumo mahiri wa utafutaji masoko.

  • Bidhaa: Siku zote bidhaa ni jambo la msingi katika mauzo mazuri. Hivyo tathmini inavyofanya  vizuri dhidi ya washindani na jitahidi kuongeza vidokezo ambavyo vitatofautisha zaidi bidhaa yako na bidhaa za watu wengine.
  • Ushuhuda: Ikiwa unatafuta masoko ya huduma ushuhuda ni muhimu kwa sababu huduma hazibebeki na wateja wanahitaji uhakika kuwa huduma yako itawafaidisha. Kwa kutoa ushahidi unaaonekana katika mfumo wa nyaraka au ushuhuda kwa wateja ni rahisi kuwapa ujasiri wateja kununua bidhaa yako.
  • Bei: Wataalamu wa masoko siku zote huwa na uwezo wa kuweka bei ambazo washindani hawawezi kulinganisha. Unaweza kufikia lengo hili kwa kuweka bidhaa yako katika mtindo ambao utakutofautisha na washindani ili kukuwezesha kupanga viwango vya bei kutokana na ubora wa bidhaa zako.
  • Eneo: Kuwa na mahali sahihi huwarahisishia wateja wako kuja kununua bidhaa kwako. Pia kutumia mitandao husaidia bidhaa husika kufika katika masoko ya kimataifa pia huwarahisishia wateja kuagiza muda wowote na kupata bidhaa hizo. Pia unaweza kupanua masoko ya bidhaa zako kwa kuuza bidhaa zako kwa wasambazaji wa rejareja wanaoongoza kwa kusambaza bidhaa zinazoendana na wewe.
  • Promosheni: Promosheni ni muhimu katika kupata mauzo zaidi.  Ni muhimu kuwajulisha wateja wako faida za bidhaa zako, bei na upatikanaji wake. Hakikisha timu yako ina ujuzi na uzoefu wa kutafuta masoko kupitia promosheni mbalimbali zitakazokuwa zikiandaliwa.
  • Watu: Watu ni muhimu ili kupata mauzo mazuri. Wateja wana maeneo mengi ya kuwasiliana na watu wao wa karibu. Hivyo ni muhimu kuhakikisha kila muwakilishi anawakilisha uzoefu mzuri kuhusu bidhaa zako. Mafunzo ya kila mara kwa watoa huduma ni muhimu ili kuweza kuhakikisha wateja wanatoka wakiwa wamefurahishwa na bidhaa pamoja na huduma.
  • Mchakato: Neno “mchakato” linahusiana na jinsi unavyosimamia shughuli zinazohusiana na wateja. Kwa mfano ubora wa mfumo wako wa simu unaweza kuwahamasisha au kuwafanya wapige simu katika kampuni nyingine ili kujipatia huduma kama hiyo unayoitoa. Kuwa na miundombinu madhubuti na watu wenye uzoefu kutaathiri mauzo kwa namna mbaya au nzuri hivyo umakini unahitajika sana.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter