Home BIASHARA Rais Samia aipa Zambia hekta 20 Bandari kavu Kwala, Pwani

Rais Samia aipa Zambia hekta 20 Bandari kavu Kwala, Pwani

0 comment 134 views

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa zawadi kwa wananchi wa Zambia kwa kutenga hekta 20 za ardhi katika Bandari Kavu eneo la Kwala mkoani Pwani.

Rais Samia amesema hayo wakati akihutubia katika maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wan chi hiyo yaliyofanyika katika viwanja vya Ikulu.

Amesema wakiongelea mgawanyo wa rasilimali, msisitizo ni kila mwananchi kunufaika huku akiongeza kuwa yeye pamoja na Rais Hakainde Hichilema ni waumini wa kuwawezesha wananchi katika maendeleo ya kiuchumi.

“Kaulimbiu ya ‘Kuchapusha Maendeleo ya Kitaifa kupitia Ugawaji wa Rasilimali’ imekuja wakati muafaka sit u kwa Zambia llakini pia kwa nchi nyingine za Afrika ikiwemo Tanzania,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema kusheherekewa kwa uhuru huo, ni kutokana na waasisi wa Mataifa hayo mawili waliamini, wakapambania walichokiamini na kuandaa mipango ya utekelezaji.

Wakati huo huo nchi hizo mbili zimedhamiria kujenga bomba jipya la gesi kutoka Tanzania hadi Zambia, kuimarisha bomba la mafuta TAZAMA pamoja na reli ya TAZARA.

Rais Samia anaendelea na ziara ya siku tatu Jamhuri ya Zambia kwa mwaliko wa Rais Hichilema ikiwa ni malengo ya kuimarisha uhusiano wa kindugu pamoja na uchumi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter