Home BIASHARA Rais wa Ethiopia aahidi ushirikiano kiuchumi

Rais wa Ethiopia aahidi ushirikiano kiuchumi

0 comment 118 views

Rais wa Ethiopia Salhe-Work Zewde amesema nchi yake ipo tayari kuongeza ushirikiano wa kibiashara na Tanzania kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi hizo mbili.

“Mimi na rais Magufuli tumekubaliana mambo mapya kwenye mahusiano katika maeneo ya biashara na uwekezaji kwa kuwa wote tunaamini kwamba waafrika wanatakiwa kuwekeza katika nchi za kiafrika,” alisema rais Zewde katika ziara yake ya siku moja nchini, wilayani Chato, Geita.

Amesema mahusiano baina ya nchi hizo mbili yanatakiwa yawe na mizizi imara ndio maana itapofika mwezi Machi au Aprili mwaka huu kitafanyika kikao cha Tume ya Ushirikiano kitakachopitia makubaliano ya mikataba yote iliyofanyika ikiwemo kuangalia maeneo mapya ya ushirikiano.

Rais Magufuli alisema ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Ethiopia umewezesha bodi ya utalii kuingia makubaliano ya kuweka matangazo ya vivutio vya utalii katika shirika la ndege la nchi hiyo jambo linaloongeza idadi ya watalii nchi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter