Home BIASHARA Sababu 3 biashara ndogo hazifiki mbali

Sababu 3 biashara ndogo hazifiki mbali

0 comment 109 views

Watu wengi huanzisha biashara wakiwa na lengo la kuziendeleza na kuhakikisha zinakuwa biashara kubwa. Asilimia kubwa ya biashara ndogo hushindwa kufikia lengo kutokana na kwamba, kadri siku zinavyokwenda, soko nalo linazidi kuwa na ushindani kutokana na biashara ambazo zinaendelea kuanzishwa kila siku. Usipokuwa na mpango maalum, unaweza kujikuta unashindwa kuendesha biashara hiyo na hatimaye kuifunga kabisa.

Hizi ni sababu kuu tatu (3) zinazopelekea biashara ndogo kushindwa kufika mbali

Utafiti kidogo unafanywa: Siku zote njia rahisi kumudu ushindani ni kujifunza na kufanya mabadiliko. Unavyozidi kujifunza na kuwaelewa wateja wako, bidhaa yako, washindani wako pamoja na mbinu unazotumia kujitangaza na kupata wateja, unakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kujua ni hatua gani unatakiwa kuchukua ili kuhakikisha kuwa hutetereki sokoni. Kwa bahati mbaya, wafanyabiashara wengi hawafanyi hivi. Baada ya kuanzisha miradi yao, wanajisahau. Ili kuifikisha biashara yako mbali zaidi unatakiwa kuendelea kujifunza, kutafiti na kuelewa soko lako kila siku.

Nguvu nyingi huelekezwa kwenye mipango mikubwa: Ukweli ni kwamba, hakuna kitu kama mafanikio ya haraka. Huwezi kuanzisha biashara leo na kutegemea kuwa itakuwa kubwa kesho. Mafanikio huchukua muda mrefu hivyo unapoweka nguvu kubwa kwenye kutengeneza mamilioni ya fedha haraka, unakosa muda wa kuendeleza kile kidogo ulichonacho kwa wakati huo kwani unakosa mpango sahihi. Imeripotiwa kuwa Jeff Bezos hakupata faida yoyote kwenye Amazon hadi mwaka 2003, ikiwa ni takribani miaka tisa tangu kuanzisha kampuni hiyo. Kinachotakiwa hapa ni kufahamu kuwa kama unaona inachukua muda mrefu kwa biashara yako kupiga hatua kubwa, basi bila shaka upo katika njia sahihi hivyo usikate tamaa.

Biashara ndogo ni ngumu kubadilika: Biashara nyingi zilizofanikiwa zimepata matokeo hayo kutokana na kujifunza, kuelewa soko na kufanya mabadiliko huku kampuni ikiendelea kukua. Ni muhimu kufanya mabadiliko yanayotakiwa kadri muda unavyozidi kwenda ili kuhama na muelekeo na soko. Kama mfanyabiashara unatakiwa kukubali mabadiliko ili uweze kusonga mbele.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter