Home BIASHARA Soko la madini lazinduliwa Chunya

Soko la madini lazinduliwa Chunya

0 comment 147 views

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila amezindua rasmi soko la madini wilayani Chunya mkoani Mbeya, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Rais Magufuli kufuatia ziara yake mkoani humo. Wakati wa uzinduzi huo, Prof. Msanjila ameeleza kuwa serikali ilitunga Sheria za madini (zikiwemo Sheria ya mamlaka ya Nchi kuhusiana na umiliki wa maliasili Namba 5 ya mwaka 2017, Sheria ya mapitio na majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi namba 6 ya mwaka 2017 pamoja na marekebisho ya Sheria ya madini sura ya 123) li kuhakikisha wananchi wananufaika na rasilimali za madini.

Pia amewataka wachimbaji wadogo kuendelea kufuata Sheria, kanuni, taratibu na miongozo inayotolewa na serikali huku akieleza kuwa, kupitia mazingira mazuri ya biashara katika sekta hiyo na ufutwaji wa tozo mbalimbali ambazo kwa pamoja zinafika asilimia 23, kutasaidia wachimbaji wadogo kutambuliwa hususani katika masoko hayo yanayoanzishwa. Aidha, ameongeza kuwa kupitia soko hilo, changamoto za utoroshaji wa madini na ukwepaji wa kodi zitapungua hivyo kurahisisha biashara ya wachimbaji na wafanyabiashara.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Prof. Idris Kikula, amesema hadi sasa masoko matano yameshafunguliwa nchini katika maeneo ya Geita, Singida, Kahama, Namanga na Chunya. Amesisitiza kuwa masoko mengine yanatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni katika maeneo ya Ruvuma, Shinyanga, Dodoma na Mbeya.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter