Home BIASHARA Taasisi 50 kushiriki kongamano la biashara

Taasisi 50 kushiriki kongamano la biashara

0 comment 116 views

Takribani Taasisi 50 zinatarajiwa kushiriki Kongamano la Biashara la Kimataifa  lililoandaliwa na Jukwaa lijulikanalo kama ‘China Trade Week’ (CTW) na kuwahusisha wafanyabiashara mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.

Kongamano hilo litakalohusisha maonesho zaidi ya bidhaa 200, litafanyika  Septemba 26 hadi 28 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.

Bidhaa hizo ni pamoja na bidhaa za kielektroniki, afya, viwanda, mavazi, urembo na ujenzi.

Kwa mujibu wa waandaaji wa kongamano hilo, Zahor Ahmed, amesema tukio hilo linalofanyika kwa mara ya kwanza nchini pamoja na mambo mengine limelenga kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na China.

“Kongamano hili limelenga kufungua  uchumi wa kimataifa kwa mataifa haya mawili na dunia nzima, biashara itakuwa mstari wa mbele kuleta maendeleo taifa,” ameeleza Ahmed.

Amebainisha kuwa kongamano  hilo ambalo Tanzania itakuwa taifa la sita kuwa mwenyeji limeshafanyika katika nchi za Kenya, Ethiopia, Afrika Kusini, Ghana na Morocco yakijumuisha maonesho ya bidhaa mbalimbali.

Mbali na faida  za  kiuchumi, kongamano hilo pia litasaidia uwekezaji na kubadilishana tamaduni zilizohusu sekta za ujenzi wa miundombinu, nishati, kilimo, chakula, sayansi na teknolojia.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter