Home FEDHA Tizameni makato ya benki, kampuni za simu: Zungu

Tizameni makato ya benki, kampuni za simu: Zungu

0 comment 426 views

Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mussa Azzan Zungu amewataka wananchi kuangalia tozo wanazokatwa na mabenki na makampuni ya simu badala ya kulalamikia makato ya serikali.

Akizungumza Bungeni Septemba 21, 2022, Zungu amesema “mimi niwaombe wananchi pamoja na sisi wabunge, unapotuma pesa tizama breakdown(mchanganuo)  ya pesa inavyoandikwa, utaona tozo ya serikali ipo chini sana na mapato wanayochukua makampuni ya simu na taasisi za fedha yapo juu zaidi ya mapato inayopata serikali”.

Amesema mabenki yanachukua pesa kubwa zaidi ya serikali kwa asilimia kubwa lakini Serikali inayojenga madarasana na vituo vya afya ndio inayolaumiwa.

Amesema jambo hilo linatakiwa kuangaliwa ni namna gani mabenki na kampuni za simu wanaweza kupunguza gharama za huduma zao.

Soma zaidi: Serikali ya Tanzania yafuta tozo miamala ya kieletroniki

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter