Parachichi ya Tanzania Sasa kuuzwa katika Soko la Afrika Kusini. Hii ni baada ya Tanzania kufanikiwa kufungua soko hilo lililokuwa limefungwa kwa takribani miaka 10.
Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram akisema “kwa wakulima wa Parachichi kwetu Hii ni taarifa njema.
Baada ya miaka mingi Hatimae baada ya Jitihada za Muda mrefu leo Tumefanikiwa kufungua Soko la South Africa
Nitumie nafasi kuwashukuru sana Wataalam wa Wizara ya kilimo na hasa kitengo cha Afya ya MIMEA
Hii ilikua ni kazi ya pamoja nawashukuru sana Sekta Binafsi nawashukuru FAO ambao tulifanya nao hii kazi Soko hili ni muhimu sana kwetu kwa zao la Parachichi hasa swala Msimu wetu na Aina ya Parachichi tunayozalisha”. Tupo hatua za Mwisho kufungua Soko la INDIA.