Kampuni ya simu ya Tecno imeendelea kuteka soko hapa nchini kutokana na bei yake kuwa nafuu ikilinganishwa na kampuni nyingine za simu. Imeelezwa kuwa Tecno inashika nafasi ya tano (5) barani Afrika katika simu zinazopendelewa zaidi.
Hivi karibuni, simu ya Tecno Phantom 9 ilizinduliwa rasmi hapa nchini na barani Afrika kwa ujumla. Simu hii imekuja na muundo wa aina yake ambao kwa hakika unavutia. Unataka kufahamu zaidi kuhusu toleo hili jipya kabisa? Sifa kamili za simu hii hizi hapa.
SIFA KAMILI:
Teknolojia:
GSM / HSPA / LTE
Uzinduzi:
Tangazo- Julai 2019
Rasmi- 25 Julai 2019 (Kwa Tanzania)
Jumba:
Ukubwa- 158.5 x 75.3 x 7.9 mm (6.24 x 2.96 x 0.31 in)
Uzito- 164.4 g (5.78 oz)
Laini- Laini mbili (Nano-SIM)
Kioo:
Mfumo- AMOLED capacitive touch screen, 16M colors
Saizi- 6.39 inches, 100.2 cm2 (~84.0% screen-to-body ratio)
Ubora- 1080 x 2340 pixels, 19.5:9 ratio (~403 ppi density)
Ulinzi wa kioo- Corning Gorilla Glass 3
Uendeshaji:
OS- Android 9.0 (Pie)
Chipset- Mediatek MT6765 Helio P35 (12nm)
CPU- Octa-core (4×2.3 GHz Cortex-A53 & 4×1.8 GHz Cortex-A53)
GPU- PowerVR GE8320
Ujazo:
Memori kadi- Micro SD, mpaka TB 1 (unaweza kuongeza mwenyewe)
Ujazo wa ndani- 128 GB, 6 GB RAM
Kamera kuu:
Kamera tatu
16 MP, f/1.8, PDAF
8 MP, f/2.4, 13mm (ultrawide)
2 MP f/2.8, (depth sensor)
Sifa zake- LED flash, HDR, panorama video 1080p@30fps
Kamera ya mbele:
Moja- 32 MP, f/2.0
Sifa Yake- HDR, video 1080p@30fps
Sauti:
Loudspeaker- Ndio (Ipo), 3.5mm jack- Ndio (Ipo)
Teknolojia Mawasiliano:
WLAN – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n/ac, dual-band, Wi-Fi Direct, hotspot
Bluetooth- 5.0, A2DP, LE
GPS- Ndio, inakuja na A-GPS
Radio- FM radio
USB- Micro USB 2.0, USB On-The-Go
Vipengele Vingine:
Sensa Fingerprint (kwenye kioo), accelerometer, gyro, proximity, compass
Betri:
Betri halitoki. Li-Ion 3500 mAh
Kitu gani kimekuvutia katika toleo hili jipya kabisa la Tecno? Umevutiwa kununua simu hii?