Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIFEDHA Utalii waingiza Bilioni 522.7 mwaka 2022/23

Utalii waingiza Bilioni 522.7 mwaka 2022/23

0 comment 49 views

Sekta ya utalii Tanzania imevunja rekodi kwa kuingiza Shilingi Bilioni 522.7 katika mwaka 2022/2023.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mohammed Mchengerwa amesema fedha hizo zimetokana na watalii 1,638,850 kutoka nje waliotembelea Tanzania kwa kipindi hicho.

“Sekta ya utalii imevunja rekodi kwa mwaka wa fedha 2022/23 kwa ongezeko ambalo halijawahi kutokea, tumshukuru sana Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha harakati za kuitangaza nchi yetu,” amesema Mchengerwa.

Ameeleza kuwa Filamu ya Royal Tour imechangia ongezeko la watalii kutoka nje ya nchi.

Amesema ongezeko hilo limeingizia taifa Sh Bilioni 522.7 ikilinganishwa na watalii 1,123,130 walioingiza Shilingi Bilioni 290.4 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 sawa na ongezeko la asilimia 45.9 ya watalii na mapato ya 80%.

“Kiwango hiki hakijawahi kutokea na matarajio yetu kitaongezeka kutoka 1,638,850 mpaka jumla ya watalii milioni tano kutoka nje.

Amebainisha kuwa sekta hiyo ambayo huchangia zaidi ya 17% ya Pato la Taifa ni miongoni mwa nguzo muhimu katika uchumi na maendeleo ya nchi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter