Home BIASHARA Uchumi uko imara- Dk. Kijaji

Uchumi uko imara- Dk. Kijaji

0 comment 170 views

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji, ameeleza kuwa uchumi wa nchi bado uko imara hata baada ya biashara 16,252 kufungwa katika kipindi cha miezi 10 mwaka huu. Dk. Kijaji amesema hayo bungeni Dodoma alipokuwa anachangia hoja ya makadirio ya Wizara ya Viwanda na Biashara na kuongeza kuwa kwa mujibu wa takwimu za serikali, biashara zilizofunguliwa ni nyingi kuliko zilizofungwa.

“Sina sababu ya kudanganya kwasababu muda wote niko ‘field’ biashara zilizofungwa na zilizofunguliwa tunazijua. Kuanzia Julai mwaka jana hadi Aprili mwaka huu, biashara zilizofungwa zilikuwa 16,252 na zilizofunguliwa ni 147,818. Huo ndio ukweli kama biashara zimefungwa TRA (Mamlaka ya Mapato) ingewezaje kukusanya kodi? Kama hali ingekuwa hivyo Tanzania ingekuwa na ‘dorminant economy’ (uchumi uliolala). Mheshimiwa Naibu Spika uchumi uko imara, uko makini na tunaendelea kutenda kwaajili ya Watanzania ndiyo maana tangu Mheshimiwa Rais (John) Magufuli aingie madarakani, hatujawahi kushuka chini ya trilioni kukusanya kodi kila mwezi, huo ndiyo uhalisia tunaoujua” amesema Kijaji.

Kuhusu mafuta kukwama bandarini, Dk Kijaji amesema kuwa muagizaji ana mamlaka ya kuthibitisha uhalali wa mafuta hayo.

“Tunachofanya ni kufuata taratibu, watanzania halali wamemuelewa Rais Dk. Magufuli. Mwaka jana ombwe kama hili la mafuta lilitokea, lakini lazima tujiulize, kwanini huwa ‘wana-target’ kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani? Sheria inasema hiki ni chakula, tuonyeshe unatuletea kutoka nchi gani? Kwa ‘original document’ (nyaraka halisi) tunataka watanzania walindwe”. Amefafanua Naibu Waziri huyo.

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter