Home BIASHARA TRA yateketeza bidhaa za Milioni 23

TRA yateketeza bidhaa za Milioni 23

0 comment 32 views

Baada ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Kilimanjaro kukamata bidhaa mbalimbali ambazo zimeingizwa nchini pasipo wafanyabiashara kufuata kanuni na taratibu, mamlaka hiyo imeteketeza bidhaa hizo zenye thamani ya takribani Sh. 23 milioni. Akizungumzia tukio hilo, Meneja Msaidizi Forodha mkoani humo Godfrey Kitundu amesema baadhi ya bidhaa zilizoteketezwa tayari zilikuwa  zimeisha muda wake wa matumizi kwa ajili ya binadamu.

Ametaja bidhaa hizo kuwa ni pamoja na mafuta ya kupikia, vipodozi, vifaa tiba na kemikali za hospitali.

Kwa upande wake, mkaguzi kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) mpakani Holili Edward Mwamilao ameeleza kuwa bidhaa hizo zingeweza kuleta athari kubwa endapo zingeingizwa sokoni.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter