Home BIASHARA Unataka kuanzisha biashara ya viatu?

Unataka kuanzisha biashara ya viatu?

0 comment 351 views

Mjasiriamali yoyote anayefikiria kuanzisha biashara ya viatu ana uhakika wa kupata wateja kwa sababu kwa namna moja au nyingine kila mtu lazima anunue viatu. Jambo la msingi katika biashara hii japokuwa wateja ni wa uhakika ni unatakiwa kujua unalenga kuuza kwa nani na kisha kuweka bei rafiki kwa kundi hilo.

Hivyo kama mfanyabiashara wa viatu ambaye ana malengo ya kufanikiwa, ni muhimu kufanya haya:

Wapinzani

Ikiwa unataka kuanzisha duka la viatu utafiti ni muhimu ili kuweza kujua mtindo upi utafaa kuvipanga viatu vyako na kuwavutia wateja na biashara yako imepanga kujikita katika viatu gani (vya bei ndogo au kubwa) kulingana na mtaji. Lakini kuna umuhimu mkubwa wa kujifunza kwa wapinzani wako ili kuwahamasisha ipasavyo wateja. Tembelea maduka ya wapinzani ili kuona namna wanavyofanya biashara, kisha orodhesha udhaifu na nguvu zao na hakikisha unafanya vizuri zaidi.

Eneo la biashara

Mara nyingi watu huvutiwa na bidhaa au mahitaji hasa pale ambapo wanakuwa wanayaona kwa urahisi. Hivyo ili kupata wateja wa kutosha jitahidi kuchagua eneo la biashara ambalo ni rahisi kufika, na kuna biashara nyingine mbalimbali zinafanyika kama vile karibu na migahawa, karibu na vituo vya usafiri nk.

Utambulisho

Siku zote wateja watakukumbuka kama kuna huduma walipata kwako na hakuna sehemu nyingine wanaweza kuipata. Hivyo kama muuzaji wa viatu hakikisha unajitengenezea utambulisho wako binafsi ambao utawafanya wateja wote wasisahau na kuwaelekeza wateja wengine kufika katika eneo lako la biashara. Kwa mfano mfanyabiashara Frank Knows amepta umaarufu mkubwa kwenye mtandao wa Instagram kwa kuuza viatu kwa Shilingi 35,000 tu bei ambayo ni bei nafuu sokoni. Kutokana na wengi kumudu bei zake, mjasiriamali huyu amefanikiwa kufungua maduka zaidi jijini Dar es salaam na mikoani.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter