Home BIASHARA Unataka kujitangaza kwa bei chee?

Unataka kujitangaza kwa bei chee?

0 comment 91 views

Masoko ni muhimu katika mafanikio ya biashara. Kampuni inapojitangaza inakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kuwafikia watu wengi hivyo kupanua wigo wake wa soko na kuongeza ya wateja wake.  Kuwa na mkakati madhubuti wa uuzaji wa bidhaa huleta mafanikio makubwa katika kampuni. Hata makampuni makubwa kama Apple huunda mikakati kila siku ya kutafuta masoko zaidi kwa ajili ya huduma au bidhaa zao.

Kama mjasiriamali siku zote baada ya kuwekeza hutaka kupata matokeo mazuri kwa kupata wateja wengi zaidi. Majukwaa kama redio, televisheni na magazeti sio kila mara yatafikisha ujumbe wako kwa wateja na huwa ni gharama kutangaza huko. Siku zote lengo kubwa la kutangaza ni kuwafikiwa wateja bila kutumia fedha nje ya uwezo wako na kupata mrejesho mzuri.

Jaribu mawazo yafuatayo ikiwa una bajeti ndogo lakini unataka kupata mrejesho mzuri wa wateja.

Andaa mashindano

Jaribu kushirikiana na makampuni makubwa kwa kuandaa mashindano yenye zawadi kubwa badala ya kuweka mashindano madogo yenye zawadi ndogo ambazo watu wachache watahamasika kushindana. Ni rahisi kushirikiana kwani kwa pamoja mtachangia gharama zinazohitajika hivyo kuandaa kitu kikubwa kwa gharama ndogo na kuwafikia watu wengi zaidi.

Himiza maudhui yanayotokana na watumiaji

Kila wakati wateja wakinunua bidhaa au huduma yako na kuitangaza katika tovuti au mitandao ya kijamii  wanakuwa wanawahamasisha watu wengine kujaribu bidhaa hiyo hata kampuni zinazojulikana zaidi mara nyingi huwa na tovuti zinazotokana na jamii na mapenzi yao katika huduma au bidhaa husika. Pia unaweza kutengeneza mashindano kujipatia masoko zaidi.

Mwambie rafiki amwambie rafiki

Kwa kutoa motisha kwa wateja ambao wanawaambia ndugu na marafiki kuhusu bidhaa au huduma yako kutakufanya uongeze wateja na kujulikana zaidi. Siku zote wateja waliolidhika na huduma yako lazima wataitangaza biashara yako. Hivyo unaweza kuwapa punguzo la bei wale wateja wanaoleta au kuwaambia ndugu jamaa na marafiki kuhusu biashara yako.

Mitandao ya kijamii

Ukilinganisha na television, redio na magazeti ni rahisi zaidi kutangaza katika mitandao ya kijamii kama facebook, LinkedIn, Instagram nk. Kwa mfano unaweza kutangaza katika facebook na instagram hata kwa 15,000, 50,000 na zaidi hivyo kulingana na bajeti yako unaweza kutangaza katika akaunti za matangazo unazo weza kumudu. Pia kuweka habari mpya katika akaunti yako kuhusiana na biashara yako kutawahamasisha watu kwani ni rahisi kwa mtu kununua anapokuwa na uhitaji nao.

Mabalozi

Wajumbe wa kampuni au mabalozi huwakilisha kampuni yako kwa kuitangaza kwa watu wengine katika mitandao ya kijamii na hata katika tovuti. Siku hizi ni rahisi zaidi kwa watu kuwa maarufu kwa vitu vidog. Hivyo kama huwezi kuwalipa watu wanaojulikana kukutangazia kwa mfano katika mitandao ya kijamii.

Kampeni za zamani

Si vibaya kutumia tena kampeni au njia ambazo zimewahi kufanya kazi zamani kwani huwezi jua itakavyowavutia au kuwahamasisha watu wengi zaidi. Sahihusha kampeni ya masoko ya awali na bidhaa na huduma za sasa. Mazoezi haya pia yatakusaidia kudumisha msimamo wa ujumbe wako.

Achana na matangazo dhaifu

Matangazo yasiyo na matokeo mazuri mara nyingi huwa ni upotevu wa fedha. Hivyo kama huoni matokeo kutokana na matangazo uliyolipia acha kutangaza ili kuepuka kuendelea kupoteza fedha zako badala yake tafuta njia nyingine, si vibaya kuwauliza watu wengine wanaofanya vizuri katika tasnia jinsi wanavyojitangaza.

Kutangaza biashara ndani ya bajeti ni jambo ambalo kila kampuni au biashara inatakiwa kufanya, haitakuwa rahisi lakini itasaidia mzunguko wa fedha. Kuna vifaa vingi na mifumo mbalimbali ya kutangaza ambayo inatumia bei nafuu au ni bure kabisa. Hivyo si vibaya kupata ushauri kutoka kwa wataalamu ili kujua njia sahihi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter